• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 2:31 PM
Wahudumu walia kuhusu ada mpya za tuk tuk

Wahudumu walia kuhusu ada mpya za tuk tuk

Na WACHIRA MWANGI

WAHUDUMU wa tuk tuk katika Kaunti ya Mombasa wamelalamika kuhusu sera mpya ya kaunti inayowahitaji kulipa Sh1,000 ili wapewe kibandiko maalumu cha kiusalama.

Kulingana na Bw Barney Ndombi anayehudumu katika eneo la Kongowea, tuk tuk hutakikana kulipiwa Sh1,200 za uegeshaji kila siku ya 15 ya mwezi.Alisema kaunti sasa inawahitaji kulipa ada mpya ya Sh1,000 kabla wakubaliwe kuhudumu wala hata kujisajili upya kwa uegeshaji mjini.

“Malalamishi yetu ni kuhusu jinsi sera zinapitishwa na kutekelezwa. Kuna jambo linaloendelea ambalo tunalitilia shaka. Hatujui mbona wanafanya hivi,” akasema Bw Ndombi.Mhudumu mwingine, Bw Tsofa Kahindi alilalamika kuwa sera hiyo ilipitishwa bila kuwepo mashauriano ya wadau.

Afisa mkuu wa kusimamia utekelezaji sheria katika idara ya usalama wa kaunti, Bw Ibrahim Basafar, alisema hatua hiyo ilichukuliwa ili kukabiliana na uhalifu ambao hutendwa na baadhi ya waendeshaji wa tuk tuk Mombasa.“Tunataka kuhakikisha tuk tuk zote zimesajiliwa pamoja na wamiliki wao ili iwe rahisi kuwapata endapo kutatokea uhalifu wowote,” akasema Bw Basafar.

  • Tags

You can share this post!

Kocha David Moyes arefusha kandarasi yake kambini mwa West...

Mbunge ataka Magoha ahojiwe kuhusu karo