• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
Korti yaagiza wadhifa wa karani wa bunge la Nairobi usalie wazi

Korti yaagiza wadhifa wa karani wa bunge la Nairobi usalie wazi

Na Collins Omulo

PENGO la uongozi litaendelea kushuhudiwa katika Bunge la Kaunti ya Nairobi baada ya mahakama kutoa amri kwamba afisi ya karani wa bunge hilo haitakuwa na mshikilizi hadi kesi iliyowasilishwa isikizwe na kuamuliwa.

Jopo la majaji watatu wakiongozwa na Roselyn Nambuye, Wanjiru Karanja na Mohamed Warsame walitoa uamuzi kwamba Edwin Gichana na Jacob Ngwele ambao wamekuwa wakizozana kuhudumu katika wadhifa huo, wasiruhusiwe kuhudumu.

Pia korti ilizuiwa mchakato wowote wa mahojiano na kuorodheshwa kwa watu ambao wangependa kushikilia afisi hiyo ya kikatiba katika bunge la kaunti.Hadi mnamo Ijumaa wiki jana, Bw Gichana alikuwa akihudumu kwenye wadhifa huo uliokuwa ukishikiliwa hapo awali na Bw Ngwele.

Hatua hiyo inamaanisha kwamba huduma muhimu zinazotekelezwa na mshikilizi wa cheo hicho sasa hazitakwepo hadi korti itoe uamuzi wa mwisho kuhusu kesi iliyoko mbele yake.Karani wa bunge ndiye mhasibu mkuu wa bunge la kaunti na huhusika na masuala yote ya kifedha ya afisi hiyo.

Pia karani ndiye katibu wa bodi ya bunge la kaunti na huhakikisha sheria zinazopitishwa bungeni zinatekelezwa vyema. Aidha ndiye humshauri spika wa bunge la kaunti kuhusu utekelezaji wa majukumu yake pamoja na madiwani kwenye masuala yanayozua utata wa kisheria.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Uteuzi wa majaji unatiliwa shaka

Corona: Uganda yasitisha kufunguliwa kwa shule