• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Corona: Uganda yasitisha kufunguliwa kwa shule

Corona: Uganda yasitisha kufunguliwa kwa shule

Na MASHIRIKA

KAMPALA, Uganda

UGANDA imesitisha mpango wa kufunguliwa kwa shule kwa madarasa chini katika shule za msingi kufuatia kuzuka kwa wimbi la pili la maambukizi ya corona nchini humo.

Katibu wa Wizara ya Elimu Alex Kakooza Jumamosi aliamuru wasimamizi wa shule wasiwaruhusu wanafunzi wa darasa la kwanza hadi tatu kurejea shuleni, pamoja na wale ambao wanakaribia kufanya mitihani ya kitaifa.

Makundi hayo ya wanafunzi yalitarajiwa kurejea shuleni kuanzia leo Juni 7, 2021 baada ya likizo ya majuma manne.

Jana, Rais Yoweri Museveni alitarajiwa kulihutubia taifa na kuweka wazi masharti mapya ya kuzuia msambao wa virusi vya corona na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.

“Wakati huo huo, wizara inafanya kazi kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu kwa lengo la kudhibiti kasi ya kuenea kwa virusi vya corona katika taasisi za masomo,” Bw Kakooza akasema.Wiki jana, Wizara ya Afya nchini Uganda iliripoti ongezeko la visa vya maambukizi ya Covid-19 shuleni.

Jumla ya shule 30 katika Wilaya 17 zilikuwa zimerekodi visa 803 na kifo kimoja kufikia Mei 18. Kufikia Ijumaa, idadi jumla ya visa ilikuwa imefika 51,006 huku wagonjwa 47,760 wakiwa wamepona na wengine 374 wakiwa wamefariki.

  • Tags

You can share this post!

Korti yaagiza wadhifa wa karani wa bunge la Nairobi usalie...

Uholanzi, Uingereza na Ubelgiji wakamilisha maandalizi ya...