• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 5:55 AM
Kupata chanjo hakumaanishi mlegeze masharti ya Covid-19  – Kagwe

Kupata chanjo hakumaanishi mlegeze masharti ya Covid-19 – Kagwe

Na SAMMY WAWERU

WAZIRI wa Afya Bw Mutahi Kagwe amesema Kenya haijashinda vita dhidi ya janga la Covid-19 licha ya chanjo kuwasili nchini.

Bw Kagwe ameendelea kuwahimiza wananchi kutilia mkazo sheria na mikakati iliyowekwa kusaidia kudhibiti msambao wa Homa ya Corona.

“Tuko katikati kupambana na janga hili na ndio maana tumeagiza chanjo,” Waziri akasema.

Alisema hayo usiku wa kuamkia Jumatano, baada ya kupokea dozi ya kwanza ya chanjo ya virusi vya corona, katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi.

“Tunahimiza kila mmoja aendelee kutuunga mkono tukabiliane na ugonjwa huu,” Bw Kagwe akasisitiza.

Shehena lililowasili nchini ni la dozi milioni 1.02 ya chanjo ya AstraZeneca, kutoka taasisi ya Serum India.

Aidha, dozi hiyo ni kati ya milioni 24 zilizoagizwa na serikali ya Kenya kuchanja asilimia 20 ya wananchi.

You can share this post!

Hit Squad kushiriki mashindano ya masumbwi DRC

Kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko atimuliwa kwa ubakaji...