• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 3:46 PM
Mafuriko yaathiri usafiri katika kaunti za Homa Bay na Kajiado

Mafuriko yaathiri usafiri katika kaunti za Homa Bay na Kajiado

GEORGE ODIWUOR Na STANLEY NGOTHO

USAFIRI umeathirika pakubwa katika vijiji viwili katika eneo la Suba, Homa Bay baada ya daraja linalounganisha maeneo hayo mawili kuharibiwa na mafuriko makubwa Jumanne asubuhi.

Wakazi wa vijiji vya Gendo na Kibwer hawawezi kusafiri kutoka upande mmoja hadi mwingine baada ya Daraja la Gendo, ambalo huviunganisha vijiji hivyo viwili kuharibika kutokana na mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha katika maeneo hayo.

Miongoni mwa wale walioathiriwa ni wanafunzi kutoka Shule ya Msingi ya Gendo, kutokana na hatari zinazowakabili wanapovuka mto huo. Iliwalazimu wengi wao kurejea nyumbani na kungoja kiwango cha maji kushuka kabla ya kujaribu kuvuka tena.

Kulingana na chifu wa Kata ya Gwassi Mashariki, Andrew Ombisa, vijiji hivyo vimekumbwa na mvua kubwa katika siku chache zilizopita.

  • Tags

You can share this post!

CECIL ODONGO: Raila hana lake kwenye vikao vya maridhiano...

Maombi yalinipa mshawasha kutaka kazi EACC – Oginde

T L