• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Mahujaji 3,000 kusafiri Mecca, Covid ikifungia wengine

Mahujaji 3,000 kusafiri Mecca, Covid ikifungia wengine

NA FARHIYA HUSSEIN

TAKRIBAN Wakenya 3,000 mwaka huu watashiriki maombi ya Hija ya kila mwaka Mecca, Saudi Arabia kuungana na Waislamu zaidi ya milioni tatu kutoka kote ulimwenguni, Baraza Kuu la Waislamu Nchini (Supkem) limetangaza.

Mwenyekiti wa Supkem Pwani, Sheikh Muhdhar Khitamy, hata hivyo, alisema walikuwa wametarajia idadi iwe zaidi ya 4,000.

Kulingana naye, huenda ikawa vizuizi vya Covid-19 vilivyowekwa na Saudi Arabia bado ni kikwazo kwa wengi.

“Umri umeathiri pakubwa idadi ya wale wanaotaka kusafiri kwa ajili ya maombi. Wanaoruhusiwa kuhudhuria lazima wawe na umri usiozidi miaka 60,” alisema Sheikh Khitamy.

Baadhi ya Wakenya waliondoka nchini wiki iliyopita huku wengine wakitarajiwa kusafiri jana Jumanne jioni.

Kundi la mwisho linatarajiwa kusafiri kufikia Julai 5.

Kwa miaka miwili iliyopita, waumini nchini walikosa kuhudhuria Hija kwa sababu idadi iliyokubaliwa Saudi Arabia ilikuwa ndogo mno.

Mahujaji watahitajika kuwa na bima ya matibabu kugharimia matibabu yao endapo wataambukizwa virusi vya corona wakiwa Saudi Arabia.

Watatakikana pia kufuata miongozo iliyowekwa na utawala wa Saudi Arabia kupunguza hatari ya maambukizi ya Covid 19.

Mbali na hayo, ni sharti wawe na chanjo dhidi ya Covid-19 ambayo imeidhinishwa na Wizara ya Afya.

Pia, watahitajika kupata chanjo nyingine za kimsingi kama vile Homa ya Manjano, Mafua ya Msimu na Neisseria Meningitides.

  • Tags

You can share this post!

Kenya Kwanza kukagua matumizi ya pesa chini ya utawala wa...

Miriam Osimbo: Nimejiwekea malengo ya kumiliki brandi ya...

T L