• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 8:50 AM
Kenya Kwanza kukagua matumizi ya pesa chini ya utawala wa Uhuru

Kenya Kwanza kukagua matumizi ya pesa chini ya utawala wa Uhuru

NA CECIL ODONGO

KINARA wa Amani National Congress (ANC), Musalia Mudavadi alisema Jumanne kuwa iwapo Muungano wa Kenya Kwanza utatwaa uongozi wa nchi Agosti 9, watafanya ukaguzi kuhusu matumizi ya fedha katika serikali ya sasa na kuchukua hatua dhidi ya watakaopatikana walishiriki uporaji.

Bw Mudavadi alidai raia hawapati thamani ya ushuru wao kwenye miradi mingi ambayo imekuwa ikitelelezwa na serikali ya Jubilee, huku watu wachache wakinufaika kwa kujitajirisha kifedha.

“Lazima tutafanya ukaguzi kwenye miradi iliyotekelezwa na serikali hii kama njia ya kusaka kiini cha deni kubwa la taifa. Kwa mfano tunataka kujua kiasi cha fedha kilichotumika kujenga bwawa la Thwake na iwapo bwawa lenyewe limenufaisha raia,” akasema Bw Mudavadi.

Alikuwa akizungumza wakati wa kongamano la kiuchumi katika eneo la Matinyani, Kaunti ya Kitui.

Aliandamana na Gavana wa Machakos Dkt Alfred Mutua na mwenzake wa Kilifi Amason Kingi.

Viongozi hao waliwashutumu Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM Raila Odinga wakisema kuwa “uongozi wao mbaya” ndio umesababisha kuvurugika kwa uchumi na kupanda kwa gharama ya maisha.

  • Tags

You can share this post!

Beth Mugo apinga uamuzi wa IEBC kutumia KIEMs pekee...

Mahujaji 3,000 kusafiri Mecca, Covid ikifungia wengine

T L