• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Makahaba wa mijini wakubali mavuno ya shambani, wahamasishana kuhusu maradhi ya zinaa

Makahaba wa mijini wakubali mavuno ya shambani, wahamasishana kuhusu maradhi ya zinaa

NA MWANGI MUIRURI

MAKAHABA katika baadhi ya miji ya hapa nchini wamezindua mpango wa kupokea mavuno ya mimea kutoka kwa wateja wao wanaotafuta huduma zao.

Hata hivyo, vipimo vya bidhaa hizo kwa huduma ya ngono, wafichua makahaba hao, ni lazima viwe sawa na thamani ya Sh200 kwenda juu.

Haya yalifichulwa Ijumaa na Mwenyekiti wa Makahaba wa eneo la Kati Bi Loise Gitau aliyezungumzia suala hilo kwenye hafla ya uhamasishaji kuhusu maradhi mapya ya zinaa katika mkahawa mmoja mjini Karatina.

Hatua ya kukubali mavuno kama malipo imetokana na ugumu wa wakulima kupata soko ikizingatiwa kwamba katika eneo hilo wengi wamepata mavuno ya kutosha. Hii ni baada ya Kaunti za Murang’a, Kirinyaga na Embu kupata baraka za mavuno ya aina mbalimbali. Hii ina maana kwamba katika kila boma kuna bidhaa za chakula za kutosha, hali inayofanya iwe vigumu kwa wakulima wengi kupata soko la bidhaa hizo.

“Kwa kuwa mavuno haya ni ya thamani sawa na pesa taslimu, tumekubaliana kwamba ni vyema tuwe tukipokea vipimo vya bidhaa hizo za shambani kama ada za kurushana roho,” akasema mmoja wa washirikishi wa makahaba katika mtaa wa Makutano.

Alisema wanaume wengi wako na mavuno lakini kufuatia soko kufurika na bei za bidhaa za mavuno kuteremka “tumeona ni lazima tuwe na mpangilio huu wa kusaidiana kwa kuwa hata tupokezwe pesa tutaishia tu kununua mavuno sokoni kulisha watoto wetu ambao tunaishi nao mijini”.

Mshirikishi huyo alisema wanapokea vipimo vya mahindi, maharagwe, mpunga na aina nyingine za nafaka.

“Kuna wale ambao wanakubali viazi, kabeji na ndizi… inategemea na ratiba na mpangilio wa kuzisafirisha bidhaa hizi hadi kwa nyumba,” akasema.

Wengi wa makahaba hao wamesema wamefurahia kwa kuwa “mara nyingi unajipata umevuna zaidi ya malipo ya huduma ukilinganisha na wakati ambapo mteja angelipia huduma kwa pesa taslimu”.

  • Tags

You can share this post!

Mpango wa kandanda Githunguri kuokoa vijana kutoka kwa kero...

Ruto na Raila washikilia misimamo mikali

T L