• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Manamba wa matatu mashakani kwa kumuibia na kumbaka mwanamke

Manamba wa matatu mashakani kwa kumuibia na kumbaka mwanamke

Na JOSEPH NDUNDA

Utingo ambaye alimburura mwanamke hadi kibanda kando ya barabara kisha kumbaka na kumuibia anakabiliwa na mashtaka ya wizi wa kimabavu na ubakaji.

Saiki Junior, 47, anadaiwa alimuibia mwanamke huyo simu yenye thamani ya Sh12,000, jaketi na Sh2,000 akitishia kumdunga kisu tumboni kama angekataa. Alitenda makosa hayo mnamo Septemba 25 akiwa mtaani Kayole.

Junior inasemekana alitumia mabavu wakati wa tukio hilo. Mwanamke huyo alikuwa ameenda kununulia dawa mwanawe ambaye aliugua ghafla usiku ndipo akakutana na Junior kwenye mzunguko wa Kayole.

Hapo ndipo mshukiwa huyo alichomoa kisu, akamkabili na kumtishia iwapo angepiga kelele.

Alimvuta kwenye kibanda kilichokuwa karibu kisha kumbaka halafu akavalia jaketi lake lililokuwa na pesa na simu na kuondoka.

Mshukiwa kisha alienda kwenye hoteli ya karibu na akaanza kujitapa kuwa jaketi ambalo alikuwa akilivalia lilikuwa la mwanamke.

Hapo ndipo mwanamke mwingine alimkabili na vurugu zikatokea kisha polisi wakaitwa na akakamatwa.

Alipofikishwa mbele ya Hakimu Mwandamizi Irene Gichobi katika Mahakama ya Makadara, Junior alikanusha mashtaka hayo.

Polisi nao waliomba mahakama iwape muda zaidi wa kufanya uchunguzi.

Ingawa hivyo, Bi Gichobi alimwachilia mshukiwa kwa dhamana ya Sh300, 000 ila akaamrisha aendelee kuzuiliwa hadi afanyiwe uchunguzi wa DNA.

Pia hakimu huyo aliamrisha idara ya mahakama impe mshukiwa huyo wakili na kusema kesi hiyo itatajwa Aprili 10, 2024.

  • Tags

You can share this post!

Pombe ya makore yatia doa Lamu, walevi wakigeuza vichaka...

Mwanamke ashtakiwa kuishi na jambazi na kukosa kuarifu...

T L