• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 5:30 PM
Mazao yanayonawiri maeneo kame yana mchango mkubwa kimaendeleo

Mazao yanayonawiri maeneo kame yana mchango mkubwa kimaendeleo

NA SAMMY WAWERU

MAENEO ya jangwa na nusu jangwa yanaunda asilimia 80 ya ardhi ya Kenya.

Mimea inayostahimili makali ya ukame na magonjwa, kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa The International Crops Research Institute for the Semi-Arid Tropics (ICRISAT), Dkt Jacqueline Hughes serikali na wadauhusika wanapaswa kuungana kuhamasisha wakazi kuikumbatia.

ICRISAT ni shirika lisilo la kiserikali linalopiga jeki wakulima nchini katika maeneo kame, na Dkt Hughes anasema itakuwa rahisi kufanikisha kilimo sehemu hizo serikali na sekta za kibinafsi zikishirikiana.

“Uhaba wa chakula na baa la njaa linalokumba wakazi maeneo hayo, yote yataangaziwa wenyeji wakihimizwa kukuza mimea yenye ustahimilivu wa juu dhidi ya ukame na magonjwa,” Dkt Hughes asisitiza.

Inajumuisha mtama, wimbi, njugu, kunde, soya, ndengu, maharagwe, mihogo, viazi vitamu, miongoni mwa mingine.

Wanasayansi na watafiti katika sekta ya kilimo, wanaendeleza mikakati kuvumbua mbegu zilizoboreshwa za nafaka kuhimili changamoto za maeneo kame, hasa kufuatia athari za mabadiliko ya tabianchi.

Dkt Hughes vilevile anahimiza haja ya maeneo hayo kukumbatia mifumo na teknolojia za kisasa kuendeleza kilimo.

Mazao yakiongezwa thamani yanateka soko lenye ushindani mkuu.

Pasilica Wanyonyi, mkulima wa wimbi, soya na mahindi katika Kaunti ya Busia, hutengeneza crackies na mandazi kwa kutumia unga wa wimbi.

Anakiri bidhaa zilizoongezwa thamani zina mapato ya haraka.

  • Tags

You can share this post!

CHARLES WASONGA: Vyuo vikuu vishirikiane na soko la ajira...

Raila kifua mbele kura ya maoni ya TIFA

T L