• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
Mbunge wa Kisumu Mashariki atishia kwenda korti kusimamisha usajili wa jeshi

Mbunge wa Kisumu Mashariki atishia kwenda korti kusimamisha usajili wa jeshi

Na ELIZABETH OJINA

Mbunge wa Kisumu Mashariki Shakeel Shabbir ametisha kwenda kortini kutaka usajili wa makurutu wa Jeshi la Kenya (KDF) usimamishwe.

Hii ni baada ya kuibuka kuwa, mamia ya vijana katika kaunti ya Kisumu wanaotaka kujiunga na KDF huenda wakazuiwa kutokana na mzozo wa mpaka kati ya Kisumu Mashariki na Kisumu ya Kati. Mzozo huo unaathiri wadi za Winam na Kajulu.

Bw Shabbir alisema kwamba kabla ya ugatuzi, wadi ya Winam ilikuwa Kisumu Mashariki. “Baada ya ugatuzi, baadhi ya wadi hizi zilisukumwa Kaunti ndogo ya Kisumu ya Kati. Hii inaweza kuathiri vijana wanaotafuta nafasi ya kujiunga na KDF,” alisema Bw Shabbir.

Vijana waliojitokeza katika shule ya msingi ya Kibos walikasirika baada ya kukatazwa kushiriki zoezi hilo.

Wengi wao walitoka wadi za Winam na Kajulu na hawakuruhusiwa kushiriki katika usajili huo.

Peter Ouma aliyekuwa akishiriki zoezi hilo kwa mara ya pili tangu 2012 aliambia Taifa Leo kwamba kwenye usajili wa makurutu wa KDF mwaka wa 2021, watu kadhaa kutoka wadi ya Winam walishiriki.

  • Tags

You can share this post!

Hofu mvua ya El Nino ikinukia huku serikali ikijikokota

Wanamapinduzi Gabon wamwachilia Bongo ‘anayeugua’

T L