• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Mbunge wa zamani kortini kwa wizi wa shamba

Mbunge wa zamani kortini kwa wizi wa shamba

Na RICHARD MUNGUTI

ALYEKUWA Mbunge wa Laikipia Antony Mutahi Kimaru ameshtakiwa kwa kuiba hatimiliki ya shamba la mlowezi raia wa Uingereza aliyeaga na ambaye mali yake nchini Kenya inasimamiwa na Dkt David Morton Silverstein, aliyekuwa daktari wa kibinafsi wa Rais hayati Daniel arap Moi.

Shamba hilo linalosimamiwa ba Dkt Silverstein na wakili mtajika George Odinga Orarop liko mjini Nanyuki kaunti ya Laikipia.

Shamba hilo ni la marehemu Livia Lepoer Trench, mlowezi kutoka Uingereza.

Katika kesi iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji, mwanasiasa huyo alishtakiwa kuiba hati ya umiliki wa shamba hilo iliyo na thamani ya Sh18.5m.

DPP kupitia kwa kiongozi wa mashtaka Bw Anderson Gikunda alisema wizi huo aliutekeleza mnamo Agosti 5 2016 katika wizara ta Ardhi aliiba hatimiliki hiyo.

Mshtakiwa alikabiliwa na jumla ya mashtaka matano alipofikishwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Milimani Nairobi Bi Martha Mutuku.

Alidaiwa alighushi makubaliano ya mauzo ya shamba hilo mnamo Agosti 3 2009 na hatimaye akijiandikia shamba hilo kwa jina lake.

Mahakama ilielezwa na kiongozi wa mashtaka Bw Anderson Gikunda kuwa mshtakiwa alimkabidhi naibu wa msajili wa mahakama ya Nyeri Bw Silas Kimeu.

Bw Kimeu ni msajili katika kitengo cha mahakama kuu ya Nyeri kinachoshughulikia masuala ya ardhi.

Bw Kimaru alimkabidhi Bw Kimeu mkataba huo wa mauzo mnamo Feburuari 5 2020.

Bw Kimaru alidai makubaliano hayo ya mauzo ya shamba hilo yaliandaliwa na kampuni ya mawakili ya Mwangi Kariuki Advocates.

Shtaka lilieleza kuwa Bw Kimaru alijua ni uwongo hakukuwa na mkataba wa mauzo wowote.

Mshtakiwa aliomba aachiliwe kwa dhamana kupitia kwa mawakili wake watatu.

Bw Gikunda hakupinga ombi hilo na hakimu aliamuru mshtakiwa alipe dhamana ya pesa tasilimu Sh300,000 pesa tasilimu.

You can share this post!

Hofu ya wanavijiji kumiliki silaha kali Kapedo

Kananu aidhinishwa kuwa Naibu Gavana wa Nairobi