• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 12:11 PM
Mhadhiri atiliwa ‘mchele’, agundua kilabuni kuna walimu tosha

Mhadhiri atiliwa ‘mchele’, agundua kilabuni kuna walimu tosha

NA LABAAN SHABAAN

MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Kenyatta (KU), anaendelea kupokea matibabu baada ya kutiliwa dawa za kupoteza fahamu katika kilabu maarufu Thika Road.

Mhadhiri huyo ambaye tumebana majina yake kwa sababu za kiusalama, inasemekana alitiliwa kwenye kinywaji tembe maarufu kama ‘mchele’ wakati akijifurahisha katika eneo hilo la burudani.

Kwenye mahojiano ya kipekee na Taifa Leo Dijitali, mhadhiri huyo alifichua kuibwa kima cha cha Sh21, 000 pesa taslimu, simu ya mkono – ndiyo rununu na kipakatalishi mnamo Ijumaaa jioni, Agosti 25, 2023.

“Ninajuta kwa kutokuwa makini,” alisema mwalimu huyo.

Alifichua kwamba alikumbana na mkasa huo wa kitapeli, alipokutana na jamaa aliyehoji walisoma pamoja shuleni na aliyeandamana na mpenzi wake.

Kulingana naye, hata aliwanunulia vileo kama ishara ya kuonyesha ukarimu.

“Mara kwa mara, nilikuwa ninaacha bia na kwenda msalani….Sikujua mambo yalivyonigeuka na baadaye kujiskia nikiwa hospitalini nikipokea matibabu,” alisimulia.

Wakati wa mahojiano, hakusita kuelezea furaha yake kwa kuwa angali hai ikizingatiwa kuwa baadhi ya dawa kupoteza fahamu husababisha maafa.

“Gari langu nalo lingali salama. Liliegeshwa katika kituo kimoja cha kuosha magari Thika Road,” alisema.

Hata hivyo, alisema baada ya kuitisha taarifa ya huduma za M-Pesa, imedhihirika pesa zilivyosambazwa na hata majina ya mhusika.

Hadi wakati wa kuchapisha taarifa hii, mhadhiri huyo hakuwa ameandikisha ripoti kwa polisi akisema atafanya hivyo atakapopata afueni.

Visa vya wanaume kutiliwa ‘mchele’ kwenye baada na maeneo ya burudani, vinazidi kushuhudiwa wahusika wakitajwa kushirikiana kwa karibu na wahudumu wa vituo hivyo vya burudani.

Waathiriwa hujipata kupoteza pesa na hata vifaa vyenye thamani.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Walevi, wamiliki baa Murang’a wampimia hewa Gavana...

Wanaharakati walaani hatua ya wanawake Lamu kufungiwa...

T L