• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Mjakazi kupimwa akili

Mjakazi kupimwa akili

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA Jumanne iliamuru mjakazi aliyewaumiza watoto wa mwajiri wake baada ya kutimuliwa kazini apimwe akili baada ya kuzua vioja kortini.

Bi Gladys Naliaka Nalianya, 22 alifika kortini akiwa ameshika viatu na mkono huku amejifunga jaketi yake kiunoni na kufunika kichwa na fulana.

Jina lake lilipoitwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Makadara Bw Angelo Kithinji alimtazama tu bila kuzugumza.

“Mbona huitiki jina lako linapoitwa na karani wa korti. Uko na shida gani. Unajua sababu umefikishwa kortini,” Bw Kithinji alimwuliza mshukiwa huyo.

Mjakazi huyo alimtazama hakimu utu. Alikuwa ametoa viatu na alikuwa anatembea miguu mitupu. Hakimu alimwuliza kiongozi wa mashtaka maoni yake kwa vile mshtakiwa hataki kusema.

“Naomba mahakama iamuru mshukiwa huyo apelekwe hospitali akapimwe ikiwa akili yake ni timamu,” hakimu alielezwa.

Bw Kithinji aliagiza mshukiwa huyo apelekwe hospitali kupimwa utimamu wa akili. Kesi inayomkabili ya kujaribu kuwaua watoto wa aliyekuwa mwajiri wake itajwe baada ya siku saba.

Naliaka alifikishwa mbele ya hakimu mkuu Bi Emily Ominde wiki iliyopita na kuagizwa azuiliwe rumande kwa wiki moja kuhojiwa.

Bi Ominde aliamuru mjakazi huyo azuiliwe katika kituo cha polisi cha Burburu hadi Machi 22,2021 atakapofikishwa kortini.

Akiwasilisha ombi Bi Naliaka azuiliwe Koplo Josephine Nduku alieleza mahakama mshukiwa alitiwa nguvuni mjini Eldoret akijaribu kutoroka mnamo Machi 13 siku mbili baada ya kuwakata kata kwa upanga watoto wawili wa mwajiri wake Bi Karen Gacheru.

“Nahitaji muda wa siku tano kumhoji mshukiwa huyu kuhusiana shambulizi hilo lilitokea katika mtaa wa Greenfield, Nairobi Machi 11,2021,” Koplo Naliaka alimweleza hakimu.

Mahakama ilielezwa wahasiriwa wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali moja jijini Nairobi. Wahasiriwa walikatwa vichwani na shingoni.

Hakimu alielezwa mshukiwa huyo ataulizwa kuonyesha polisi kule alitupa silaha alizotumia kuwajeruhi watoto hao.

Alipoachishwa kazi, mahakama , ilielezwa mjakazi huyo aliapa kuwasababishia maumivu watakayoishi nayo milele.

  • Tags

You can share this post!

JAMVI: Karata za Uhuru zinavyohatarisha Mlima Kenya...

Pigo kwa Spurs fowadi Kane akiumia katika sare ya 2-2 dhidi...