• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 5:55 AM
MKU yaendesha kongamano la kibiashara

MKU yaendesha kongamano la kibiashara

Na LAWRENCE ONGARO

CHUO Kikuu cha Mount Kenya (MKU), na kituo cha YUNUS Centre, zimefanya kongamano la kumi la pamoja la Social Business Academic Conference (SBAC).

Kongamano hilo lililoendeshwa kwa njia mseto ya mtandaoni na pia kuhudhuriwa moja kwa moja, liliwaleta pamoja watafiti, wasomi na wanafunzi kutoka ulimwenguni kote ambapo walijadiliana maswala ya ubunifu na biashara.

Kongamano hilo liliendesha kwa siku tatu mfululizo kuanzia Novemba 4, 2021 hadi Novemba 6, 2021.

Kongamano hilo lilifinguliwa na msomi anayetambulika kutoka Bangladesh Profesa Mahammad Yunus.

Msomi huyo anatambulika sana kwa maswala ya kibiashara, uchumi, benki na haki za kibinadamu.

Profesa Yunus anatambulika kutokana na ubunifu wake wa kuzindua benki ya Grameen, na kuanzisha biashara za chini.

Naibu Chansela wa MKU Profesa Deagratius Jaganyi, alitaja chuo hicho kama cha kimataifa kwa hatua ambazo kimepiga kufikia sasa.

“Tunaweza kujivunia hatua ambayo tumepiga ya kukabiliana na kuangamiza umaskini, njaa na kuhifadhi mazingira kwa njia zote,” alifafanua msomi huyo.

Alisema ushirikiano uliopo kati ya kituo cha Social Business Centre cha Prof Yunus, ni hatua kubwa ya kujivunia kwa sababu italeta maendeleo makubwa.

Kongamano lililofanyika mwaka huu kupitia kituo cha Yunus liliangazia mtaala wa masomo kuhusu biashara na utafiti kwa lengo la kuangazia eneo la Afrika Mashariki na Kati, huku yaliyozungumzwa yakijumuisha maoni ya wasomi kutoka ulimwengu mzima.

Maswala mengi yaliyoangaziwa ni kuhusu jinsi ya kuboresha elimu katika eneo la Afrika Mashariki.

Wakati wa ufunguzi wa ukumbi wa Mwai Kibaki Convention Centre hivi majuzi, Naibu Chansela Profesa Jaganyi alisema una uwezo wa kujaza watu 2,000 kwa wakati moja kwa maswala ya masomo.

“Tunajivunia ukumbi huo kama chuo kwa sababu tutaweza kujumuisha watu wanaoendesha mikutano ya pamoja, mikutano ya mameneja, na wanafunzi kwa jumla.

Alisema chuo hicho kinatafuta mbinu ya jinsi ya kupokea mapato ya kifedha ili kuendesha mikutano huku pia wakijaribu kujitambulisha kuwa na raslimali za kisasa na vifaa vya kuvutia wageni.

Kwa muda mchache sasa ukumbi huo umewaleta pamoja wasomi wengi kwenye makongamano kadha ya hadhi ya kimataifa.

Ukumbi huo umetajwa kama wa kimataifa kwa sababu vifaa vilivyoko ndani ni vya kisasa vinavyoambatana na viwango vya kimataifa, vikiwa na vyumba vingi tofauti vyenye nafasi ya watu 40 kwa kila chumba kwa wakati mmoja.

  • Tags

You can share this post!

Kesi dhidi ya mbunge wa Wajir mashariki yatamatishwa

Serikali ya wakaidi wa sheria

T L