• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
MKU yakabidhiwa cheti cha ubora kutoka KEBS

MKU yakabidhiwa cheti cha ubora kutoka KEBS

NA LAWRENCE ONGARO

CHUO Kikuu cha Mount Kenya (MKU) kimepokea cheti kutoka kwa Halmasharuri ya Ubora Nchini (KEBS) iliyotambua namna chuo hicho kinavyotoa huduma na kuendesha majukumu yake.

Profesa David Serem aliye mwenyekiti wa kamati ya chuo hicho alisema cheti cha lSO 9001 kinaeta mabadiliko mengi chuoni kwa kukiweka katika ramani ya dunia.

MKU ina matawi kadha katika eneo la Afrika Mashariki na Kati.

“Tunatarajia vyuo vingine kadha vitajitahidi ili viweze kutambulika na kupata ISO,” alieleza Prof Serem.

Hafla hiyo ya kufana ilifanyika katika mkahawa mmoja mjini Kiambu, ambapo mgeni wa heshima alikuwa Mhandisi Zacharia Lukorito, ambaye ni mkurugenzi wa KEBS.

Chansela wa MKU Profesa John Struther aliyehudhuria hafla hiyo na mkewe alisema muda wote amehudumu katika chuo hicho mengi mazuri yameonekana.

Alisema kazi nzuri iliyofanywa chuoni ndiyo ilichangia chuo hicho kupata cheti cha utambulisho cha ISO.

“Kiwango kizuri cha masomo na jinsi wanafunzi wanavyonyesha bidii ni baadhi tu ya sababu zilizochangia MKU kupokea cheti hicho,” alifafanua Prof Struther.

Alisema kumekuepo na ushindani mkali katika vyuo vikuu tofauti ulimwenguni lakini wao kupata cheti cha ISO 9001 ni sawa na kupata ngao ya “kututambulisha kama chuo kilichojiimarisha.”

Bi Esther Ngari alisema cheti cha ISO 9001 kilipatikana chuoni huko kwa mara ya kwanza mwaka wa 2015.

“Hiyo imetokana na kutambulika kikamilifu kutokana na jinsi tumejipanga kwa kutoa elimu ya juu kupitia maswala ya utafiti na ubunifu huku chuo kikijitambulisha vilivyo katika ramani ya dunia,” alieleza Bi Ngari.

Dkt Jane Nyutu mwanzilishi wa chuo hicho alipongeza uongozi wa chuo hicho ukiongozwa na Prof Deogratius Jaganyi kwa kufanya juhudi ya kuleta cheti hicho.

“Ninatambua mwongozo ambao umechukuliwa na KEBS kwa kutushikilia tangu 2012, tulipopokea cheti cha ISO 9001 kwa mara ya kwanza,” alieleza Dkt Nyutu.

Alipongeza chuo hicho kwa jumla hasa wahadhiri na wanafunzi kwa kukiweka mahali kilipo hadi sasa.

Dkt Vincent Gaitho alisema usimamizi wa chuo hicho na wafanyakazi wengine ni nguzo muhimu.

“Ningependa kuwapongeza wasimamizi na wafanyikazi wote kwa kuonyesha uzalendo wa kufanya MKU ipige hatua,” alisema Dkt Gaitho.

  • Tags

You can share this post!

Liverpool wafungua kampeni za EPL 2022-23 kwa sare ya 2-2...

TAHARIRI: Wanasiasa wamemaliza yao, uamuzi sasa ni wako

T L