• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:07 PM
Mkuu wa shule ya msingi kizimbani kwa kupora Sh2 milioni

Mkuu wa shule ya msingi kizimbani kwa kupora Sh2 milioni

NA JAMES MURIMI

MWALIMU mkuu katika Kaunti ya Laikipia, Ijumaa aliachiliwa na Hakimu Mkazi wa Nanyuki kwa dhamana ya Sh1 milioni pesa taslimu au mdhamini wa Sh2 milioni, baada ya kukana shtaka la kufuja Sh2.251 milioni.

Lenard Mbotela anayesimamia Shule ya Msingi ya Ilmoro eneo bunge la Laikipia Kaskazini alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Nanyuki Lisper Nyaga na kushtakiwa ka kupora pesa zilizonuiwa kutumika katika ujenzi wa shule moja ya upili katika eneo hilo.

Anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Septemba 25 na Desemba 17, 2021 katika benki ya KCB, tawi la Nanyuki.

Pesa hizo zililenga kutumika kufadhili ujenzi wa Shule ya Upili ya Ilmotiok.Mbotela alitia saini kama akaunti za shule hiyo kama mweka hazina wa kamati ya ujenzi wake.

Alikana mashtaka na kuachiliwa huru kwa dhamana.

“Kesi hiyo itatajwa mnamo Juni 14, 2022 na kusikilizwa mnamo Juni 20, 2022. Mshtakiwa anafaa kupewa stakabadhi zote zinazohusiana na kesi hii,” Hakimu akaamuru.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Umekuwa msimu wa Ligi Kuu yenye pandashuka tele

Mudavadi ahofia kubaki kwa mataa kisiasa baada ya Agosti 9

T L