• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Msongo wa mawazo unasababisha vijana kuota mvi mapema -utafiti

Msongo wa mawazo unasababisha vijana kuota mvi mapema -utafiti

Na LEONARD ONYANGO

Ikiwa wewe ni kijana na tayari umeanza kuwa na nywele nyeupe kichwani, kuna uwezekano kwamba wewe ni mwathiriwa wa tatizo la msongo wa mawazo (stress).

Ripoti ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Columbia Vagelos, ulibaini kuwa msongo wa mawazo wa mara kwa mara humfanya mtu kuwa na mvi kichwani mapema licha ya kuwa na umri mdogo.Watafiti hao walihusisha mvi na mabadiliko ya kisaikolojia.

Kwa kawaida, ubongo hutumia nguvu nyingi wakati mtu ana fikiria sana. Hali kama hiyo huweza kusababisha mtu kuota mvi.Kulingana na watafiti hao, kasi ya kichwa kupata mvi inaweza kupungua endapo mwathiriwa atapata muda wa kutulia, kupumzika na kulala bila kuwa na mawazo mengi.

“Tafiti zetu zinadhibitisha kuwa kuzeeka ni mchakato wa kibaolojia. Kuota mvi kichwani ni jambo ambalo linawezabadilishwa kwa muda,” alisema mwandishi mkuu wa Chuo Kikuu cha Columbia Dkt Martin Pcard.

  • Tags

You can share this post!

Watu 400,000 wanakumbwa na njaa Tigray-UN

PCEA yapiga marufuku siasa makanisani