• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 7:05 PM
Watu 400,000 wanakumbwa na njaa Tigray-UN

Watu 400,000 wanakumbwa na njaa Tigray-UN

Na AFP

NEW YORK, Amerika

UMOJA wa Mataifa (UN) umesema zaidi ya watu 400,000 wanakumbwa na njaa katika eneo la Tigray, Ethiopia, kutokana na mapigano yanayoendelea.

Kwenye mkutano wake wa kwanza kuhusu mgogoro nchini humo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) lilisema zaidi ya watoto 33,000 wanakumbwa na utapiamlo.Maafisa wa umoja huo walisema kuwa karibu watu 1.8 milioni wako kwenye hatari ya kukumbwa na baa la njaa kutokana na mapigano hayo yaliyodumu kwa miezi minane.

Vile vile, walionya kuhusu uwezekano wa kuchipuka kwa mapigano mapya licha ya uwepo wa mkataba wa kuyasitisha.Serikali ya Ethiopia ilitangaza kusitisha mashambulio yake dhidi ya eneo hilo Jumatatu.

  • Tags

You can share this post!

Wahamiaji 43 wafariki mashua ikizama

Msongo wa mawazo unasababisha vijana kuota mvi mapema...