• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Mtandao wa BrighterMonday wapendelewa zaidi na watafutaji ajira nchini, yasema ripoti

Mtandao wa BrighterMonday wapendelewa zaidi na watafutaji ajira nchini, yasema ripoti

NA WINNIE ONYANDO

JUKWAA la mtandao la kutafuta ajira la BrighterMonday limeibuka kuwa maarufu na lenye kupendwa na mamilioni ya wanaotafuta ajira.

Zaidi ya watu milioni 4.6 wanaotafuta kazi na waajiri zaidi ya 150,000 wanapendelea jukwaa hilo kutokana na huduma zake bora.

Jukwaa hilo ni sehemu ya kampuni ya African Talent Company na linatumika katika nchi za Nigeria, Ghana na Uganda.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Hilda Kabushenga Kragha alisema kuwa, kampuni hiyo itapanua huduma zake ili kuleta pamoja watu wengi zaidi wanaotafuta ajira na waajiri.

“Tuna uwezo wa kuwezesha waajiri kupata watu waliona tajriba hitajika ili kuboresha sekta ya ajira nchini. Waajiri watapata orodha ya majina ya watu waliobobea katika sekta hitajika. Hii itawawezesha kuwaajiri watu waliona uwezo wa kuwasaidia kuendeleza na kuimarisha kampuzi zao,” akasema Bi Kragha.

Kadhalika, kampuni hiyo pia inanuia kutoa mafunzo za kidigitali kwa watu wanaotafuta ajira ili kuwawezesha kupata tajriba husika na kuwaweka katika mstari wa mbele kupata ajira.

  • Tags

You can share this post!

Rais wa UAE Khalifa bin Zayed Al Nahyan afariki

ICC yamruhusu wakili Gicheru kutumia ushahidi

T L