• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:31 PM
Mwanamume aliyekiri kuiba mkate na maziwa Naivas kuhukumiwa juma lijalo

Mwanamume aliyekiri kuiba mkate na maziwa Naivas kuhukumiwa juma lijalo

NA JOSEPH NDUNDA

MAHAKAMA ya Makadara itamhukumu mwanaume, 30 aliyekiri kuiba bidhaa katika duka la jumla la Naivas, tawi la Embakasi, Jumanne ijayo.

Hakimu Mwandamizi Mkuu wa Makadara, Bi Mary Njagi, aliamuru Ambrose Kipkoech Towett, azuiliwe korokoroni hadi Jumanne, Oktoba 24, polisi watakapowasilisha bidhaa hizo kortini kama ushahidi.

Towett jana alikubali kosa la kuchukua mkate, maziwa na mafuta ya kupika kabla ya kujaribu kuondoka bila kulipa.

“Alitoa risiti aliyoitumia miezi miwili iliyopita nje ya mji wa Nairobi kama ithibati. Mashine za duka zilijulisha walinzi na kumsimamisha,” alisema Victor Opiyo, Meneja wa Tawi hilo.

Mashtaka yanasema alichukua kilo 14 za sukari, lita mbili za mafuta ya kupikia, boflo ya mkate, maziwa miongoni mwa bidhaa zingine kinyume cha sheria.

Anakabiliwa na shtaka lingine la kupatwa na mali ya wizi baada ya kukamatwa akiondoka supamaketi hiyo.

Inadaiwa kwamba Towett alienda kwa supamaketi hiyo iliyoko eneo la Kobil, mtaa wa Pipeline akijifanya mteja ambapo alichukua bidhaa hizo na kuziweka ndani ya mfuko na kujaribu kuondoka bila kuzilipia.

Alipokuwa anapita langoni, mashine maalum za kunasa wizi zilikiriza na kufanya askari wa langoni kumnyaka mara moja.

Alipohojiwa na maafisa wa usalama wa duka hilo hakuweza kuelezea kwa nini alikuwa anaondoka bila kulipia bidhaa.

Meneja wa tawi hilo Victor Opiyo na mlinda lango wa duka hilo wameorodheshwa kama mashahidi pamoja na maafisa wawili wa polisi lakini hawatatoa ushahidi kwa sababu Towett ameshakiri mashtaka.

  • Tags

You can share this post!

Viongozi Pwani kufanya kazi na Rais Ruto bila miegemeo ya...

Magavana wataka Inspekta Jenerali amuombe Mwangaza radhi...

T L