• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:12 PM
Mwanamume ashtakiwa kuhusisha Jenerali Ogolla na maandamano ya Azimio

Mwanamume ashtakiwa kuhusisha Jenerali Ogolla na maandamano ya Azimio

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAJESHI wa zamani ameshtakiwa kuchapisha habari za uwongo katika mitandao ya kijamii akidai Mkuu wa Majeshi (CDF) Jenerali Francis Ogolla alikuwa akifadhili maandamano ya muungano wa Azimio yaliyofanyika Julai 2023.

Franklin Opiyo Ogonji alishtakiwa mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama ya Milimani Ben Mark Enkhubi kwa kuchapisha habari za uwongo na kumfedhehesha Jenerali Ogolla.

Ogonji aliyetimuliwa kazini baada ya kushtakiwa kwa kuiba lori la vyakula vinavyopelekewa maafisa wa jeshi wakiwa kazini alikabiliwa na mashtaka manne ya kueneza habari za uwongo katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook kwa jina Frank Mac Poyoz.

Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh50,000.

Wakati huo huo, Seneti leo Agosti 28, 2023 inafanya kikao maalum kushughulikia masuala mbalimbali ya dharura ikiwemo hoja ya kuhalalisha Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo.

Kikao hicho kiliitishwa na Spika wa bunge hilo Amason Kingi kupitia tangazo kwenye gazeti rasmi la serikali, toleo la Agosti 25, 2023.

“Kikao hicho maalum kitafanyika katika ukumbi wa Seneti, majengo ya bunge, Nairobi, Jumanne Agosti 29, 2023 kuanzia saa tatu na nusu za asubuhi (9.30 am),” Spika Kingi akasema.

Hoja ya kuhalalisha Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo yenye wanachama 10, watano kutoka Kenya Kwanza na watano kutoka Azimio la Umoja-One Kenya, ilipitishwa katika Bunge la Kitaifa wiki moja iliyopita.

Kamati hiyo, inayolenga kuleta maridhiano kati ya mirengo hiyo miwili inaongozwa na wenyeviti wenza, kiongozi wa wengi bungeni Kimani Ichung’wa (Kenya Kwanza) na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka (Azimio).

Katika kikao hicho maalum, maseneta pia watajadili Mswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Mabadiliko ya Tabianchi ya 2023 na Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma wa 2023.

Miswada hii miwili ilipitishwa na Bunge la Kitaifa juma moja lililopita na sharti ipate idhini ya Seneti kabla ya kutiwa saini na Rais William Ruto ili iwe sheria.

Wakati huu, maseneta wako katika likizo fupi na watarejelea vikao vya kawaida mnamo Jumanne Septemba 5, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Mwili wa mwanamume wapatikana kwenye tanuri la uchomaji...

Mrembo njia panda baada ya wanaume wawili kudai ndio baba...

T L