• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
Mzozo kuhusu mpango wa kukabidhi Mumias Sugar usimamizi mpya

Mzozo kuhusu mpango wa kukabidhi Mumias Sugar usimamizi mpya

Na Benson Amadala

MPANGO wa kukabidhi msimamizi mpya wa kiwanda cha sukari cha Mumias kinachozongwa na matatizo ya kifedha, umeibua mgawanyiko tena kati ya wanasiasa kutoke eneo la Magharibi.

Kampuni ya Devki wiki jana ilijiondoa katika mpango wa kuchukua usimamizi wa kiwanda hicho kutokana na pingamizi za wanasiasa hasa Seneta wa Kaunti ya Kakamega Cleophas Malala.

Ingawa wengi wa wanasiasa wamekuwa kimya kuhusu hatima ya kiwanda hicho kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu, mpango wa kukabidhi Devki usimamizi huo, umeibua cheche kali kati ya wabunge wa vyama vya ODM, ANC na Jubilee.

Kutokana na hilo, mbunge wa Lugari, Bw Ayub Savula jana alisema amefaulu kuwafikia wanasiasa wote na wanapanga kuandaa mkutano na Waziri wa Kilimo, Bw Peter Munya na Afisa Mkuu Mtendaji wa benki ya KCB ambayo ni mrasimu, Joshua Oigara wiki hii kujadiliana kuhusu suala hilo la usimamizi mpya wa kiwanda hicho.

Gavana wa Kakamega, Wycliffe Oparanya naye ametofautiana na msimamo wa Bw Malala, akisema KCB ina haki ya kukabidhi msimamizi mpya kiwanda hicho ili kuendeleza juhudi za kukifufua.

You can share this post!

TAHARIRI: Uhifadhi mazingira usiwe ni siku moja

Kipchirchir aweka rekodi mpya ya Eldoret Marathon