• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 12:03 PM
Nahitaji miaka 3 kuifahamu vyema idara – Jaji Mkuu Martha Koome

Nahitaji miaka 3 kuifahamu vyema idara – Jaji Mkuu Martha Koome

Na RICHARD MUNGUTI

JAJI Mkuu Martha Koome amesema kuwa itamchukua miaka mitatu ili kuielewa vyema Idara ya Mahakama.

.Jaji Mkuu Koome, aliyekabidhiwa rasmi afisi Jumatatu, alisema Idara ya Mahakama inakabiliwa na matatizo chungu nzima na “nitahitaji miaka mitatu kuweka mikakati ya kuyatatua.”

“Kama mnavyojua mimi ni mgeni katika hii ofisi na idara ya mahakama ni kubwa. Nitakuwa pia ninaongoza tuma ya huduma za idara ya mahakama JSC sawia na kuwa rais wa Mahakama ya Juu,” alisema Jaji Koome akijibu maswali ya wanahabari.

Alisema suala la kutoapishwa kwa majaji 41 na Rais Kenyatta kumechangia pakubwa baadhi ya matatizo yanayoikumba idara ya mahakamna.

“Kila tatizo liko na suluhu mumu humu. Kwa hivyo nitawasiliana na asasi zote husika katika kusaka suluhu ya shida zinazokumba mahakama,” alisema Jaji Koome.

Jaji huyu mkuu mpya alisema hayo alipomwapisha Bw Morris Kimuli aliyeteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta kufuatia kutimuliwa kwa Dorothy Jemator KimengenchBw Kimuli aliteuliwa na chama cha wanasheria nchini kutwaa mahali pa Bi Kimengich anayehudumu katika mashirika mengine mawili.

Wanachama wengine wa kamati hiyo ya kuteua makamishna hao ni Dkt Elizabeth Muli, Gideon Solonka, Elizabeth Meyo, Rev Joseph Ngumbi na Dkt Faradim Abdalla.

Kamati hii ya itateua wanne makamishna kuungana na Bw Wafula Chebukati (mwenyekiti), Prof Yakub Guliye na Boya Molu.

Makamishna hao wanne wa IEBC watachukua nafasi zilizoachwa wazi kufuatia kujizulu kwa Consolata Nkatha, Roselyn Akombe, Paul Kurgat na Margaret

Mwachanya.Bw Kimuli aliteuliwa na chama cha wanasheria nchini LSK baada ya kuzuka mtafaruku kati ya rais wa chama hicho Nelson Havi na afisa mkuu wa LSK Bi Mercy Wambua.

You can share this post!

Aliyejeruhiwa akivuka feri Likoni kulipwa Sh418,000

Walimu hatarini kukosa nyongeza ya mishahara