• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 AM
Ndege ya kwanza yapeleka miraa baada ya mkataba wa marais

Ndege ya kwanza yapeleka miraa baada ya mkataba wa marais

NDEGE ya kwanza kupeleka miraa Mogadishu iliondoka Jumapili asubuhi wiki moja baada ya Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Somalia Hassan Mohamud kutia saini mkataba wa kuuza zao hilo nchini humo.

Kurejelewa kwa biashara hiyo kuliacha hata kabla ya Mamlaka ya Ndege Nchini Somalia (SCAA) kutoa taarifa rasmi ya kuruhusiwa kwa ndege zinazosafirisha khat (miraa) kutua mjini Mogadishu.

Katika mtandao wake rasmi wa Facebook Waziri wa Kilimo Peter Munya alisema, “Ndege ya kusafirisha Miraa imeondoka Kenya kuelekea Mogadishu leo (Jumapili) asubuhi.”

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Kuuza na Kukuza Miraa (Nyamita) Kimathi Munjuri alisema walisafirisha tani tano “kujaribu jinsi soko lilivyo.”

“Ni ukweli ndege ya kwanza ya kusafirisha mizigo iliondoka na tani tano za miraa Jumapili asubuhi,” alithibitishha Munjuri.

Hata hivyo aliongeza kusema, “Tunatoa wito kwa mamlaka ya ndege ya Somalia itoe taarifa rasmi kuhusu kuzinduliwa upya kwa safari za ndege zinazobeba miraa.”

Aliongeza kusema, taarifa rasmi kutoka kwa mamlaka ya ndege Somalia bado haijatolewa.

Mwenyekiti huyo aliipongeza serikali kwa bidii iliyoweka kuhakikisha biashara hiyo imerejelewa baada ya kusitishwa vita vilipozuka jijini Mogadishu.

  • Tags

You can share this post!

WALIOBOBEA: Musikari aliiga Kibaki, akakabili ufisadi vikali

Oleksandr Zinchenko sasa mali rasmi ya Arsenal

T L