• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
Hisia mseto zatolewa kufuatia kauli ya Ngilu ‘kukejeli’ mavazi ya Ruto

Hisia mseto zatolewa kufuatia kauli ya Ngilu ‘kukejeli’ mavazi ya Ruto

Na WANGU KANURI

WATUMIAJI wa mtandao wa kijamii wa Twitter wameonyesha hisia mseto baada ya Gavana wa Kitui Charity Ngilu kuchapisha picha ya Naibu Rais William Ruto akiwa amevalia mavazi ya kitamaduni na kisha kudai kwamba ni kama alisaka huduma za mganga.

Kwenye picha zilizomfanya Bi Ngilu kutoa matamshi ya aina yale, Naibu Rais alikuwa amejiunga na wakazi wa kaunti ya Turkana katika sherehe za sita za Tobong’u Lore.

Isitoshe, Dkt Ruto alikuwa pamoja na magavana kutoka kaunti za Turkana, Uasin Gichu na Baringo.

Vuta nikuvute iliyosheheni mtandaoni ilionyesha misimamo ya wanaomshabikia Naibu Rais kwa upande mmoja na wanaomshabikia kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga kwa upande mwingine.

“Turkana ina utamaduni wa kipekee na ambao wao hulinda kwa fahari. Naibu Rais, huheshimu utofauti wa utamaduni na aliwaunga wenyeji wa Turkana katika kusherehekea mila zao. Ni vibaya kuwaona watu wakikejeli na kutumia maneno kama uganga,” akasema Milicent Omanga.

“Ni kwa nini wanasiasa wengine pamoja na Wakenya huchafulia wenzao jina huku wakidhani wanajijengea sifa? Ni vyema tufanye siasa zinazoongozwa na masuala sio hisia za watu,” akaeleza Fred Kathanga.

“Hii ni tukio la kimila si uchawi. Waganga wanaweza pia kuvalia suti. Unapaswa kufutilia ulichosoma kutoka kwa wamishenari,” akaandika David Ndii.

“Ukweli usemwe. Hakuna utamaduni hapa. Huu ni uganga. Wao hutabiri yajayo kwa kushauri vizimwi,” akasema Gideon_Kitheka.

“Hakuna uganga wowote hapa. Huu ni utamaduni wa wenyeji wa jamii pana ya Turkana. Viongozi wanapaswa kuacha kuwapotosha watu kwa kuzungumza yaliyo kweli na kuheshimu tamaduni za watu wengine,” akaandika Kariuki Wanjahi.

“Huu ni uganga sisi sio wajinga,” akasema Brian Luka.

“Unapaswa kuwaomba msamaha wakazi wa Turkana kwa kunasibisha utamaduni wao na uganga,” akaeleza Makau Muli.

You can share this post!

ODM kumenyana na UDA Bondeni

Wiper yajitenga na Gideon Moi kuhusu kuunga Raila 2022

T L