• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
Ngilu aweka ushirika na NHIF kuwezesha familia 200,000 za mapato ya chini kugharimia matibabu

Ngilu aweka ushirika na NHIF kuwezesha familia 200,000 za mapato ya chini kugharimia matibabu

Na Kitavi Mutua

SERIKALI ya Kaunti ya Kitui imeanza kusajili zaidi ya familia 200,000 kwenye Mpango wa Afya kwa Wote (UHC) kama njia ya kuhakikisha wana bima ya kugharimia matibabu na kuwaepushia gharama kubwa wanapougua.

Gavana wa Kitui Charity Ngilu jana alizindua mpango huo wa afya ambao utahakikisha hata familia maskini inajivunia bima ya matibabu.

Hii itasaidia hasa wakati huu baadhi ya hospitali zimekuwa zikiwazuilia wagonjwa wanaoshindwa kulipia gharama ya matibabu.

Tayari familia maskini 85,000 kutoka wadi zote 40 zimetambuliwa na zitanufaika na mpango huo ambao Gavana Ngilu aliufikia kwa ushirikiano na Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF).

Tayari baadhi ya familia za Kaunti ya Kitui zimekuwa zikinufaika na Bima iliyoanzishwa na Bi Ngilu maarufu kama (KCHIC) ambayo inawawezesha kupata matibabu nafuu katika hospitali ya kaunti hiyo. Ingawa hivyo, kupitia huu ushirikiano na NHIF, kaunti sasa itawalipia Sh3,000 kila mwaka ambazo ni nusu za pesa wanazostahili kulipa.

‘Tumekuwa tukitumia bima ya KCHIC ambayo imehakikisha kuwa wakazi wa kaunti ya Kitui wanapokea matibabu kwenye hospitali za kaunti zetu. Kupitia ushirikiano na NHIF sasa watatumia hospitali na vituo vya kiafya zaidi ya 8,000 kote nchini,’ akasema Bi Ngilu.

You can share this post!

Wenye jinsia mbili walia kubaguliwa wakisaka huduma

Sturridge apata hifadhi katika kikosi cha Perth Glory...