• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Wenye jinsia mbili walia kubaguliwa wakisaka huduma

Wenye jinsia mbili walia kubaguliwa wakisaka huduma

Na Wycliffe Nyaberi

WATU wenye jinsia mbili nchini wanataka mageuzi yatakayohakikisha uhuru wao na haki zao za kimsingi zinalindwa.

Kundi la watu hao linasema hakuna usawa wowote baina yao na watu wa kawaida, hasa wanapotafuta huduma za serikali.

Wamesema tatizo kuu linalowakumba ni unyanyapaa dhidi yao pale raia wanapogundua wana maumbile tatanishi.Kwa kuwa mtu hachagui atakavyoumbwa, wameomba hamasisho za kina kufanywa ili kuelimisha umma kuhusu hali zao kuwavumilia.

Mtu mwenye jinsia mbili kulingana na ripoti ya jopokazi kuhusu sera, uhalisia na mageuzi katika taasisi za utawala ni yule asiyejulikana ikiwa yeye ni mke au mume.

Mara nyingi ana viungo vyote vya siri japo kiungo kimoja huonekana kuwa na nguvu kuliko kingine.Kulingana na takwimu za sensa ya kitaifa ya mwaka 2019, Kenya ina jumla ya watu 1,524 ambao wana jinsia mbili. Kaunti ya Kisii ina jumla ya 38 ya watu hao, huku ikiorodheshwa katika nafasi ya saba kitaifa.

Sensa hiyo ilifanya Kenya kuwa taifa la kwanza kabisa barani Afrika kuwahi kukusanya deta za watu wenye jinsia mbili pia.

Kwenye warsha lililoandaliwa mapema wiki hii katika kaunti ya Kisii, mahuntha hao walieleza changamoto wanazozipitia wakitafuta kuhudumiwa.

Miongoni mwa hitaji walilosema linawakera mno ni ukosefu wa kutambua kuwa kunayo jinsia ya tatu katika fomu za kutafuta vyeti vya kuzaliwa kwa watoto waliozaliwa na maumbile hayo tata.Ubaguzi mwingine waliolalamikia ni katika elimu na wanapotaka kuchukua mikopo ambayo wanasema huwawia vigumu kupata kutokana na maumbile yao.

You can share this post!

Serikali yaanza kujenga barabara ya lami kuinua hadhi ya...

Ngilu aweka ushirika na NHIF kuwezesha familia 200,000 za...