• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
NMG yapiga jeki Mbogolo ECD kwa msaada wa vitabu

NMG yapiga jeki Mbogolo ECD kwa msaada wa vitabu

NA ALEX KALAMA

ZAIDI ya wanafunzi 70 kutoka shule ya chekechea ya Mbogolo ECD Center iliyoko wadi ya Ganda katika eneobunge la Malindi kaunti ya Kilifi wamenufaika na msaada wa vitabu kutoka kwa shirika la habari la Nation Media Group.

Akizungumza wakati wa kupokea vitabu hivyo mnamo Ijumaa waziri wa elimu katika serikali ya kaunti ya Kilifi Clara Chonga alipongeza NMG kwa kujitolea na kufadhili shule hiyo ambayo inakubwa na uhaba wa vitabu na pia ina upungufu wa madarasa.

“Tunashukuru sana Nation Media kwa kujitolea kwenu kushirikiana na serikali ya Kilifi katika kuimarisha elimu ya chekechea, na huu msaada ambao mmetoa hii leo naomba isiwe mwisho bali tuzidi kushirikiana zaidi ili kuhakikisha mtoto wa Kilifi anapata elimu bora,” alisema Bi Chonga.

Hata hivyo waziri huyo wa elimu wa kaunti alidokeza kuwa serikali ya kaunti hiyo inajitahidi kufanya kila iwezalo li kuhakikisha kwamba watoto wa shule za chekechea wanasoma katika mazingira bora.

“Najua tuko na changamoto nyingi ambazo zinatukumba hapa Kilifi lakini vile vile sisi kama kaunti tumejitahidi ili kuona ya kwamba matatizo haya tumeweza kuyatatua. Kwa sasa tumeanzisha mpango wa lishe shuleni wale watoto wote ambao wako shule za chekechea za umma wanapewa uji ili waweze kusoma vizuri,” alisema Bi Chonga.

Kwa upande wake afisa mkuu wa mauzo kutoka shirika la Nation Media Group Philbert Mdindi aliwahimiza wazazi kujitahidi kupeleka watoto wao shuleni ili kupata elimu,akisema hiyo ndio njia pekee ya itakayowasaidia kujikwamua kutoka katika Lindi la umaskini.

“Wazazi najua hali ya uchumi imekuwa ngumu lakini nawaomba jinyimeni kidogo ili angalau muweze kusomesha hawa watoto wenu,kwa sababu hawa watoto mukiwasomesha vizuri wataweza kuja na kubadilisha hii hali ya maisha mlio nayo kwa sasa.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo alisema  shule hiyo bado inahitaji kuboreshwa kwani inakumbwa na changamoto nyingi ikiwemo miundo msingi.

“Bado tunahitaji msaada kwa sababu hii shule  iko na darasa moja peke yake,na ukiangalia kwa sasa tuko na wanafunzi sabini na saba.

Hawa wanafunzi tuko nao ni wengi hawastahili kusoma katika darasa moja, lakini kwa sababu hatujapata lingine inabidi tu wafinyane hapo ili mradi wapate kusoma kwa hivyo tunaomba mtusaidie,” alisema.

  • Tags

You can share this post!

Ufukuaji makaburi Shakahola waendelea, walioangamia ni 391

EPRA yafeli kutoa afueni kwa Wakenya

T L