• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 6:55 PM
Ufukuaji makaburi Shakahola waendelea, walioangamia ni 391

Ufukuaji makaburi Shakahola waendelea, walioangamia ni 391

NA ALEX KALAMA

ZAIDI ya maiti 50 zimefukuliwa kufikia sasa kwenye awamu ya nne ya ufukuaji wa makaburi kuondoa miili watu waliozikwa katika hali tatanishi ndani ya msitu wa Shakahola, Kaunti ya Kilifi.

Hii ni baada ya maiti saba zaidi kufukuliwa mnamo Ijumaa na hivyo kuchangia waliothibitishwa kufariki kuongezeka kwa hadi jumla ya watu 391.

Kulingana na taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani Rhoda Onyancha, hakuna mtu yeyote aliyeokolewa wala kukamatwa kwa kuhusishwa na mauaji hayo katika operesheni iliyoendeshwa Ijumaa.

Shughuli ya kuendelea kutafuta miili zaidi kutoka kwa msitu huo inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi.

Mhubiri Paul Mackenzie anahusishwa pakubwa na vifo vya watu hao. Alikamatwa na angali kizuizini.

  • Tags

You can share this post!

Ajali: Wawili waokolewa mawimbi yakitatiza utafutaji wa...

NMG yapiga jeki Mbogolo ECD kwa msaada wa vitabu

T L