• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
NTSA yatoa mafunzo mapya kwa madereva

NTSA yatoa mafunzo mapya kwa madereva

Na WANGU KANURI

MAMLAKA ya Usalama Barabarani (NTSA) imetangaza mikakati ya kuanzisha mtaala wa kielektroniki wa kuwatahini madereva wote nchini Kenya.

Mamlaka hiyo kwa ushirikiano na Umoja wa Ulaya chini ya programu ya Usalama Barabarani, inanuia kuboresha mitihani inayofanywa na Wakenya wanapopokea mafunzo ya uendeshaji magari.

Kulingana na ripoti iliyotolewa mwaka huu ili kutathmini vifo vilivyoshuhudiwa barabarani mwaka wa 2021, barabara ya Outering iliyoko jijini Nairobi ilirekodi vifo 44, idadi hii ikiwa ya juu zaidi.

Barabara ya Waiyaki Way ilirekodi vifo 38, huku barabara ya Mombasa Road na Northern Bypass ikirekodi vifo 29. Southern Bypass ilirekodi vifo 28 huku barabara hizi tano zikirekodi idadi kubwa Nairobi.

Kwa mujibu huo, Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiria kuwa watu milioni 2.5 hufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabara. Nchini Kenya, zaidi ya watu 3000 huaga dunia baada ya kuhusika kwenye ajali za barabarani.

Hata hivyo asilimia 85 za maafa hayo husababishwa na tabia za watu kama vile uendeshaji gari mtu akiwa mlevi, uendeshaji gari kwa kasi na kutokuwa na maarifa kuhusu kuzingatia usalama barabarani.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Itakuwa aibu raia mwenye njaa kuombwa kura

Serikali mbioni kuangamiza mbung’o waharibifu Kwale

T L