• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
OCS wa kituo cha Garissa aachiliwa kwa dhamana akikana mashtaka ya mauaji

OCS wa kituo cha Garissa aachiliwa kwa dhamana akikana mashtaka ya mauaji

Na FARHIYA HUSSEIN

AFISA mkuu wa kituo cha polisi Kaunti ya Garissa Michael Munyalo ameachiliwa kwa dhamana ya Sh1 milioni mnamo Alhamisi.

Afisa huyo aliyefika mbele ya jaji Abdida Ali Aroni katika Mahakama Kuu ya Garissa alikana mashtaka ya mauaji.

Munyalo alishtakiwa kwa mauaji ya mtu mmoja aliyekuwa na umri wa miaka 28 na akatambuliwa kuwa ni Morris Kimathi.

Tukio hilo linasemekana kutokea mnamo Mei 16 katika barabara ya Bula Sheikh ndani ya maskani ya burudani wakati Afisa Munyalo na maafisa wengine walikuwa wakipiga doria katika mji huo saa za jioni wakati wa kafyu.

Sababu kuu ya kile kilichotokea wakati wa tukio hilo bado haijajulikana.

Afisa huyo alikamatwa mara moja baada ya wakazi kuandamana katika mji wa Garissa, Jumatatu, Mei 17.

Afisa Munyalo alifikishwa mbele ya korti siku ya Alhamisi, Mei 20, ambapo Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuomba muda zaidi wa uchunguzi na afisa huyo kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Madogo akisubiri uchunguzi.

Walakini, upande wa mashtaka leo ulikuwa umepinga dhamana ikisema kuwa iwapo mshtakiwa ataachiliwa atakua tishio kubwa kwa usalama wake na wengine.

Lakini jaji huyo alipinga ombi hilo na kutaja kuwa sio sababu tosha ya kumnyima mshtakiwa dhamana.

Kesi hiyo itasikilizwa Julai 7, 2021.

  • Tags

You can share this post!

Inter Milan wamteua Inzaghi kuwa kizibo cha kocha Antonio...

Katiba Institute yapinga uteuzi wa majaji 34 na kuachwa nje...