• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Patrick ‘Jungle’ Wainaina asema ni vyema Kawira Mwangaza apewe muda

Patrick ‘Jungle’ Wainaina asema ni vyema Kawira Mwangaza apewe muda

NA LAWRENCE ONGARO

ALIYEKUWA Mbunge wa Thika Bw Patrick ‘Jungle’ Wainaina amependekeza wanasiasa wanaowania viti vya ugavana kwa tikiti ya kujitegemea (Independent), walindwe kutokana na kubanduliwa vitini mapema.

Alisema viongozi waliochaguliwa kwa tikiti ya kujitegemea hasa magavana wako katika njia panda kwani hawana mtetezi kamili.

“Ninatoa mfano wa Gavana wa Meru Bi Kawira Mwangaza ambaye madiwani wa kaunti hiyo waliwasilisha katika seneti uamuzi wao wa kumbandua uongozini wakidai hana uadilifu kazini,” alisema Bw Wa Jungle.

Aliyasema hayo kijini Kihara, KiambuĀ  alipozindua ufunguzi wa nyumba za Ribazi.

Alisema ingefaa magavana waliochaguliwa wapewe muda kama wa miaka miwili hata mitatu kutekeleza wajibu wao ili waangaliwe kama wameedesha wajibu wao ipasavyo.

“Hiyo tabia ya madiwani kuungana pamoja na kutaka kumng’oa gavana ni hatari na inaangazia taswira mbovu hata mbele ya wapigakura. Ni vyema kupewa muda wa kufanya kazi kikamilifu kabla ya kutoa vitisho hivyo,” alifafanua Bw Wa Jungle.

Gavana Mwangaza aliwabwaga wapinzani wake kadha akiwemo wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) ambacho kilikuwa kikiwika maeneo hayo.

Kwa hivyo Wa Jungle anapendekeza magavana wawe wakipewa muda wa kutosha ili wajitambulishe vilivyo kwa wapigakura na waonyeshe kuwa wanaweza kutumikia wananchi kwanza.

“Lakini baada ya gavana Mwangaza kufikishwa katika Bunge la seneti kufanyiwa mahojiano kuhusu makosa yake, alipatikana kuwa hana hatia yoyote,” akasema Bw Wa Jungle.

Anasema wabunge na masenata wanastahili kupitisha sheria ambayo itamlinda gavana anayechaguliwa kuongoza kaunti yake.

Anasema baadhi ya viongozi huhiari kujisimamia kwenye uchaguzi badala ya kujiunga na vyama vingi ambavyo hutumia njia nyingi za kuteua wagombea viti vya uongozi huku kukiwa na malumbano mengi ndani ya vyama hivyo.
  • Tags

You can share this post!

Malindi: Wanawake wafanya kazi za sulubu kwa bidii kukabili...

Kagame akataa zigo la wakimbizi wa DRC

T L