• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 12:42 PM
Pesa za wazee ziwafae wajane

Pesa za wazee ziwafae wajane

Na MHARIRI

KENYA inapoungana na ulimwengu leo kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wajane, yafaa tukumbuke kuwa hakuna mtu anayependa kufiwa na mpenzi wake.

Mauti yanapoikumba nyumba, mpenzi mmoja hubaki na mzigo mkubwa wa kukubali majaaliwa. Mara nyingi wanaume huweza kujikusanya haraka na hata kuoa tena.Lakini mambo huwa tofauti kwa wanawake wajane, ambao mara nyingi hujikuta wakinyanyaswa, kudhulumiwa, kutukana na kunyima haki zao za kimsingi.

Familia za wanaume waliokufa – hasa dada (mawifi) na kaka – huwa mstari wa mbele kuongeza kuendeleza dhuluma hizi.

Wakati mwingine hata mjane hushutumiwa kuhusika na kifo cha mumewe. Shutuma hizo zinapotokea, hutoa fursa nzuri kwa jamaa wa marehemu kumpokonya mjane mali yote, ambayo kisheria ni urithi wa watoto kama wapo, au wa mjane mwenyewe, kama hakuwa amezaa.

Kutokana na tamaa ya mali, ndugu wa marehemu hujigawia magari, nyumba, shamba na vyote ambavyo huenda kaka yao alishirikiana na mkewe kuvitafuta.Ingawa kuna wanawake wanaopata ujane wakiwa wangali wachanga, idadi kubwa ya wajane wanaoteseka ni wakongwe, wasiokuwa na watu wa kuwatunza.

Serikali kupitia mpango wa Inua Jamii imekuwa ikiwafaa wakongwe walio na zaidi ya miaka 65 kwa mgao wa Sh2,000 kwa mwezi.

  • Tags

You can share this post!

Watoto wapewe basari bila ubaguzi – Magoha

Brazil kumalizana na Colombia leo usiku