• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 9:17 PM
Pigo kwa agizo la Ruto kuruhusu ukataji miti kwenye misitu

Pigo kwa agizo la Ruto kuruhusu ukataji miti kwenye misitu

NA SAM KIPLAGAT

MAHAKAMA ya Mazingira na Masuala ya Ardhi imesitisha agizo la Rais William Ruto kuondoa marufuku ya ukataji miti kwenye misitu.

Marufuku hayo yalikuwa yamewekwa mwaka 2018.

Akitoa agizo hilo, Jaji Oscar Angote vile vile amesitisha mpango wa serikali kutaka kurejesha mfumo unaofahamika kama Shamba System, hadi kesi iliyowasilishwa na Chama cha Wanasheria Nchini (LSK) isikilizwe na kuamuliwa.

Mfumo wa shamba uliruhusu raia kutunza misitu wakati miti ikiwa midogo huku wakiruhusiwa kupanda mimea ya mavuno kama mahundi na maharagwe.

LSK inasema hatua zote za kisheria hazikufuatwa kuondoa marufuku hayo na wala athari kwa misitu inayolindwa kupitia chapisho kwenye gazeti rasmi la serikali.

“Kabla ya kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi hii, agizo linatolewa kuwazima washtakiwa binafsi au maajenti, watumishi, wafanyakazi au watu wengine wanaofuata maagizo yao ili wasitoe leseni au vibali vya kuruhusu ukataji wa miti na rasilimali nyingine za misitu,” limesema agizo la mahakama.

Rais Ruto alitangaza kuondolewa kwa marufuku hayo Julai 2, 2023, akihutubia wakazi wa Molo katika Kaunti ya Nakuru.

Alisema hatua hiyo ililenga kuzifaa familia na watu wanaoishi karibu na misitu.

“Agizo halikutoa ithibati za kisayansi, utafiti, sera, athari kwa mazingira au ushirikishi wa umma haswa kwa wanaoishi karibu na misitu inayoweza kuharibiwa kufuatia agizo hilo la serikali,” LSK ikasema.

Aidha iliongeza kuwa Rais Ruto aliondoa marufuku hayo kwa kauli ya mdomo tu bila kufuatisha na chapisho kwenye gazeti rasmi la serikali.

  • Tags

You can share this post!

Wakulima waonywa kuhusu kemikali nyingi

Jinsi Al-Shabaab walivyo tishio kwa walimu

T L