• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Wakulima waonywa kuhusu kemikali nyingi

Wakulima waonywa kuhusu kemikali nyingi

NA SAMMY WAWERU

WANASAYANSI na watafiti katika masuala ya kilimo wameibua hofu kuhusu matumizi kupita kiasi ya kemikali katika mimea.

Kilimo cha mahindi ndicho kinaongoza kwa matumizi ya kemikali kukabiliana na kero ya wadudu na magonjwa.

Akizungumza jana, Jumanne, katika mkutano wa Baraza la Wahariri Nchini (KEG) na wadau husika katika sekta ya kilimo, Dkt James Karanja, mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo cha Mimea na Uimarishaji Mifugo (KALRO) tawi la Kabete alionya kwamba taifa lisipokuwa makini huenda suala hilo likawa janga.

Kongamano hilo la Jijini Nairobi, pia lilileta pamoja Wanasayansi wanaohamasisha kuhusu mifumo ya Bayoteknolojia kuboresha shughuli za kilimo na kudhibiti bidhaa.

Dkt Karanja ambaye ni mtaalamu wa uzalishaji mahindi na mtafiti mkuu katika mpango wa TELA (ushirikiano wa sekta ya umma na kibinafsi kutafiti bridi bora ya mahindi), alisema kwa sasa ikilinganishwa na miaka 10 iliyopita, kiwango cha kemikali kinachotumiwa shambani kimepanda maradufu.

Huku wengi wakiendeleza dhana kuwa chakula kilichozalishwa kupitia ubunifu wa Bayoteknolojia hususan mazao ya GMO ndicho huchangia Saratani, Dkt Karanja asema kemikali katika kilimo ndizo kiini kikuu.

  • Tags

You can share this post!

Data: Serikali yaipiga breki Worldcoin

Pigo kwa agizo la Ruto kuruhusu ukataji miti kwenye misitu

T L