• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Simanzi mwanamuziki Kiambukuta akifa

Simanzi mwanamuziki Kiambukuta akifa

Na JOHN ASHIHUNDU

MWANAMUZIKI maarufu Josky Kiambukuta Londa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ameaga dunia jana Jumapili jijini Kinshasa.

Kiambukuta alifariki hospitalini mjini humo akitibiwa baada ya kuugua kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa wa kiharusi.

Alijipa umaarufu mkubwa akiwa na kundi la TP OK Jazz la marehemu Franco Luambo Lwanzo Makiadi.

Msanii huyo aliyejiunga na TP OK Jazz mnamo 1974 alikuwa miongoni mwa viongozi walioendesha kundi hilo kwa miaka minne baada ya kifo cha Franco mnamo 1989 kabla ya mvutano uliobuka mnamo 1994 kati ya wanamuziki hao na familia ya marehemu Franco.

Kiambukuta, Simaro Lutumba na Ndombe Opetum walikuwa miongoni mwa wanamuziki waliojitenga na kuunda kundi la Bana OK.

Baadaye, Kiambukuta alihamia jijini Paris nchini Ufaransa lakini akarejea nyumbani mnamo 2019 kuhudhuria mazishi ya Lutumba.

Risala za rambirambi ziliendelea kumiminika kupitia mitandao ya kijamii kwa jamaa na marafiki wa aliyefariki akiwa na umri wa miaka 72.

You can share this post!

Wafanyabiashara Thika wapokea Sh4 milioni za Uwezo Fund

Wanajeshi na wahudumu wa afya Nakuru kuchanjwa