• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 7:50 AM
TUONGEE KIUME: Usichotakiwa kufanya ukiwa mwanamume usiye na ajira

TUONGEE KIUME: Usichotakiwa kufanya ukiwa mwanamume usiye na ajira

Na KELVIN KAGAMBO, ripota Mwananchi Communications Limited

Katika kitabu chake cha The End of Jobs, milionea kijana Taylor Pearson ameandika, “kwa enzi hizi za matumizi makubwa ya mashine na intaneti, ajira yako ni kitu kinachoweza kupotea kufumba na kufumbua, kwa hiyo ujasiriamali ni salama zaidi ya ajira.”

Nasema katika enzi hizi za matumizi makubwa ya mashine na intaneti na siasa chafu za Afrika, hakuna uthabiti wowote katika ajira wala ujasiriamali.

Kama unavyoweza kuamka ukaambiwa kampuni iliyokuajiri inapunguza wafanyakazi, ndivyo unavyoweza kuambiwa Serikali imepiga marufuku uuzwaji wa nguo za mitumba, wakati huo wewe una shehena ya mashati ya mitumbo huko stoo.

Ninachojaribu kukwambia ni kwamba, siku yoyote unaweza kuwa huna chanzo cha kupata pesa tena.

Na mwamamume bila pesa ni mwanamume dume suruali. Na hili sio mpaka uambiwe, hapana! Litaanzia kwako mwenyewe, taratibu utaanza kujiona unapoteza ‘hamu’ ya kuwa mwanamume.

Sasa kila mwanamume anajua cha kufanya asipokuwa na kazi, ni kimoja tu, kutafuta kazi nyingine, lakini wengi hatujui nini hatutakiwi kufanya tusipokuwa na kazi, na leo ndiyo tutazungumzia hicho.

  1. Usikae nyumbani; hataka kama huna mahali pa maana pa kwenda, hakikisha haukai nyumbani kabisa. Amka asubuhi, nenda zako hata kwenye mjengo, kaangalie jinsi shughuli zinafanyika siku nzima. Ikifika jioni rudi nyumbani kama umetokea ofisini.

Hufanyi hivi ili majirani wasijue kibarua kimeota nyasi, hapana. Unafanya hivi ili nyumbani wasikuzoee, kwa sababu kwa mazoea tu, unaweza kushangaa mkeo anakutuma ukalete mwiko, na ukiona umeshafika huku, jua pointi inayofuata inakuhusu.

  1. Usiwe na mtazamo hasi kwa mkeo; mwanamume ukiwa huna pesa, huna kazi, uko nyumbani tu, unakuwa kama kamusi, kila neno linalosemwa, wewe una tafsiri yake.

Mkeo akisema, “Baba Brian, naomba muangalie mtoto mara moja niende dukani.” Wewe utasikia kasema, “Baba Brian, kwa sababu huna hela na huna kazi, umekaa hapa siku nzima unapoteza muda kwa kuangalia TV utadhani unalipwa, sasa kaa na mtoto, mimi naenda dukani kununua cha kupika hapa, ili nipike, ule, ujaze hilo tumbo, upate nguvu ya kushika rimoti na kuendelea kubadilisha chaneli, na kupoteza muda zaidi.”

Kuanzia hapo utamjibu vibaya, atakujibu vibaya pia, mtajibizana, matokeo yake hakuna hata kitakachopikika kabisa.

Kwa hiyo ili usifikie huku, ni vyema sana kujitahidi kutokuwa na mtazamo hasi kuhusu mkeo.

Yaani, usiwe na mtazamo hasi kiasi kwamba hata akisema jambo baya kukuhusu, wewe lichukulie kwa upesi.

  1. Usijifanye kila kitu kiko sawa; kwa sasa wewe bwana huna kazi, labda huna pesa vilevile, kwa hiyo lazima kuna vitu havitaenda kama kawaida nyumbani na hili ni jambo la kutarajia. Kitu ambacho hutakiwi kufanya wakati kama huu ni kuigiza kama kwamba kila kitu kiko sawa. Utaharibu.
  • Tags

You can share this post!

Mabilioni yamwagika kukabili mabadiliko ya tabianchi Afrika

Biashara ya nyama inachangia mazingira kuzorota, kongamano...

T L