• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:04 PM
Uhuru aongoza mkutano wa marais wa EAC kujadili mzozo wa DRC na Rwanda

Uhuru aongoza mkutano wa marais wa EAC kujadili mzozo wa DRC na Rwanda

NA CHARLES WASONGA

RAIS Uhuru Kenyatta Jumatatu, Juni 20, 2022, aliongoza mkutano wa marais sita wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Mojawapo wa ajenda kuu wa mkutano huo uliofanyika katika Ikulu ya Nairobi, ni mzozo wa kidiplomasia katika ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Rwanda.

Hali hiyo imechangiwa madai ya DRC kwamba Rwanda inaunga mkono waasi wa M23 ambao wanalaumiwa kwa mashambulio nchini humo.

Mkutano wa Jumatatu ulihudhuriwa na marais Paul Kagame (Rwanda), Yoweri Museveni (Uganda), Evariste Ndayishimiye (Burundi), Salva Kiir Mayardit (Sudan Kusini) na Felix Tshisekedi (DRC).

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliwakilishwa na Balozi wa taifa hilo nchini Kenya John Stephen Simbachawene.

Mwishoni mwa mwaka 2021, uhusiano kati ya Rwanda na DRC ulizorota baada ya Bw Tshisekedi kumsuta mwenzake Kagame kwa kuunga mkono waasi ambao wamekuwa wakisababisha mashambulio katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Rwanda imelaumiwa kwa kuunga mkono waasi wa M23 ambao wanapigana na vikosi vya usalama wa serikali ya DRC. Serikali ilikana madai hayo.

Lawama hizi ziliongeza uhasama katika ya mataifa hayo na kupelekea DRC kupiga marufuku ndege za shirika la ndege la RwandaAir kuhudumu katika anga yake.

Kama hatua ya kulipiza kisasi, serikali ya Rwanda pia ilipiga marufuku safari zote za ndege zake kuelekea miji ya Kinshasa, Lubumbashi na Goma.

Mnamo Ijumaa Juni 17, 2022, DRC pia ilifunga mpaka wake na Rwanda kuhusiana na madai kuwa mwanajeshi wake mmoja alipigwa risasi na kuuawa katika makabiliano kati yao na wanajeshi wa Rwanda.

  • Tags

You can share this post!

Wito waandishi wa habari wamakinike kuelekea uchaguzi mkuu...

Shirika la Heifer lahimiza vijana wawe mstari wa mbele...

T L