• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Uingereza yapongezwa kwa kuwa na msimamo chanya kuhusu matangazo ya CGTN

Uingereza yapongezwa kwa kuwa na msimamo chanya kuhusu matangazo ya CGTN

NA MASHIRIKA

Habari zilizotolewa na vyombo vya habari vya Uingereza zinasema, mamlaka ya usimamizi wa mawasiliano ya Uingereza Ofcom inakubali kwamba, huduma za Shirika la Kimataifa la Televisheni la China CGTN ziko chini ya usimamizi wa Ufaransa, hali ambayo inamaanisha kuwa matagazo ya CGTN yanaweza kurejeshwa nchini Uingereza, kufuatia Makubaliano ya Televisheni ya Kuvuka Mipaka ya Ulaya.

Msemaji wa CGTN amesema shirika hilo litawasiliana na pande husika, ili kuthibitisha hali ilivyo, na kuhimiza kurejea kwa matangazo yake nchini Uingereza. Amesema Ofcom inakaribishwa na kupongezwa kwa kuwa na msimamo chanya na wa haki kuhusu jambo hili.

Msemaji huyu amesisitiza kuwa, ikiwa chombo cha kimataifa cha habari, CGTN inatoa ripoti kwa msimamo wa ukweli, haki na uwiano, na kuendelea kutoa matangazo yake kwa watazamaji wa Uingereza kunalingana na maslahi ya umma ya nchi hiyo.

  • Tags

You can share this post!

JAMVI: Mjane atakuwa mbunge wa kike wa kwanza Kisii?

JAMVI: Kilio IEBC ikiendelea na chaguzi ndogo bila ya...