• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Ujenzi wa daraja la kidijitali kupima uzani wa magari

Ujenzi wa daraja la kidijitali kupima uzani wa magari

NA LABAAN SHABAAN

MAMLAKA ya Kitaifa Kuhusu Usalama wa Barabara Kuu Nchini (KeNHA), imetangaza kufungwa kwa sehemu ya barabara ya Southern Bypass kati ya makutano ya Langata na Ngong, Jijini Nairobi.

Kupitia notisi kwa umma, KeNHA iliweka wazi kuwa barabara hiyo itafungwa kwa muda wa siku 27 ili kupisha ujenzi wa Daraja la Kidijitali Kupima Uzani wa magari, maarufu kama Virtual Weighbridge.

“Kufungwa kwa barabara hiyo kutaanza Desemba 27, 2023 hadi Januari 23, 2024. Ili kupunguza usumbufu kwa wasafiri, kufungwa huku kutahusisha leni moja ya kila barabara kwa wakati mmoja,” inasema sehemu ya notisi ya KeNHA, kupitia ukurasa wake rasmi wa X (awali Twitter) mnamo Jumatano, Desemba 27, 2023.

Taarifa hiyo ilitiwa saini na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Mhandisi Kung’u Ndung’u.

Bw Kung’u ameomba watumiaji wa barabara kuwa waangalifu watakapokaribia eneo litakalofungwa.

Aidha, aliwataka maderava kuwa makini na kuheshimu alama za barabara na maelekezo yatakayotolewa.

Kituo cha Kidijitali Kupimia Uzani hunasa takwimu kutoka kwa sensa na kamera, kuainisha magari na baadaye kutuma data kwa uchakataji katika kituo cha udhibiti.

Hivi, mfumo huo hubainisha uzani wa magari na yaliyomo katika vyombo vya usafiri.

KeNHA inafanya ukarabati huo ili kupunguza visa vya ajali barabarani vinavyosababishwa na madereva wanaovunja sheria.

Itategemea daraja hilo kudhibiti visa vya magari kubeba mizigo kupita kiasi, hali ambayo huharibu miundomsingi ya barabara.

Ramani ya sehemu za barabara ya Southern Bypass zitakazofungwa. PICHA | HISANI

 

  • Tags

You can share this post!

Krismasi: Alivyorambwa kwenye baa akijigamba mbele ya...

Vidosho wa ‘mchele’ wafurika Ziwa Naivasha...

T L