• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 2:36 PM
Ujerumani kuonana na Uingereza huku Ureno wakipepetana na Ubelgiji katika hatua ya 16-bora

Ujerumani kuonana na Uingereza huku Ureno wakipepetana na Ubelgiji katika hatua ya 16-bora

Na MASHIRIKA

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

MABINGWA watetezi wa Euro, Ureno, walifuzu kwa hatua ya 16-bora ya Euro licha ya kuambulia sare ya 2-2 dhidi ya Ufaransa kwenye mchuano wa mwisho wa Kundi F mnamo Jumatano usiku.

Cristiano Ronaldo alifunga mabao mawili ya Ureno kupitia penalti na kufikia rekodi ya magoli 109 iliyowekwa na Ali Daei wa Iran kati ya 1993 na 2006.Ufaransa ambao ni mabingwa wa dunia walifungiwa mabao yao kupitia Karim Benzema wa Real Madrid.

Ushindi huo wa Ufaransa almaarufu ‘Les Bleus’ ulihakikisha kwamba wanakamilisha kampeni za Kundi F kileleni kwa alama tano, moja pekee kuliko Ujerumani na Ureno. Hungary walivuta mkia wa kundi lao kwa alama mbili.

Ronaldo aliwafungulia Ureno ukurasa wa mabao katika dakika ya 30 baada ya kipa Hugo Lloris kumkabili visivyo Danilo. Hata hivyo, Benzema alisawazisha mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya Nelson Semedo kumwangusha Kylian Mbappe ndani ya kijisanduku.

Ushirikiano mkubwa kati ya Benzema na Paul Pogba mwanzoni mwa kipindi cha pili uliwapa Ufaransa bao la pili kabla ya Ronaldo kusawazisha mambo kunako dakika ya 60.Ronaldo alifikisha mabao 20 kwenye soka ya bara Ulaya na hivyo kumpita aliyekuwa mvamizi wa Ujerumani, Miroslav Klose.

Nyota huyo sasa anajivunia mabao 48 kutokana na mechi 45 zilizopita ndani ya jezi za Ureno. Amepachika wavuni mabao matano kutokana na mechi tatu zilizopita za Euro. Ronaldo ndiye anapigiwa upatu wa kutawazwa Mfungaji Bora wa Euro mwaka huu. Huku Ureno wakipepetana na Ubelgiji katika hatua ya 16-bora, Ufaransa watachuana na Uswisi jijini Bucharest.

 

  • Tags

You can share this post!

Ujerumani kuvaana na Uingereza kwenye hatua ya 16-bora ya...

Fahamu nani atakutana na nani kwenye droo kali ya hatua ya...