• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 7:55 AM
Ushindani mkali vyuo vikuu vikiingia debeni leo

Ushindani mkali vyuo vikuu vikiingia debeni leo

ZAIDI ya wajumbe 500 wa Muungano wa Wafanyakazi wa Elimu katika Vyuo Vikuu (UASU) leo watashiriki uchaguzi wenye ushindani mkali kuwachagua viongozi wapya katika ukumbi wa Nakuru Athletics Club.

Wawaniaji 46 watashiriki kinyang’anyiro hicho cha kuwania nyadhifa 10.Chuo Kikuu cha Kenyatta kilicho miongoni mwa vitengo vikuu zaidi kikiwa na wajumbe 20, hakitashiriki uchaguzi huo baada ya chaguzi zake kufutiliwa mbali na korti kutokana na ukiukaji wa sheria.

Hii ni mara ya kwanza tangu muungano huo kubuniwa ambapo unashiriki chaguzi zake za kitaifa katika mji huo ulio eneo la Bonde la Ufa.Wadhifa wa mwenyekiti ambao unatarajiwa kushindaniwa vikali, umevutia mgombea wa kike kutoka Nakuru, Bi Grace Nyongesa, ambaye amejikakamua kuwa mwenyekiti wa kwanza kabisa mwanamke wa Uasu, ikiwa atashinda chaguzi hizo katika jaribio lake la kwanza la kugombea kiti hicho.

“Grace Nyongesa anazua mkondo mpya katika chaguzi za Uasu na ndiye mabadiliko tunayotaka katika nyadhifa za juu za uongozi,” alisema Dkt Patrick Murerwa, katibu mwandalizi wa Uasu katika Chuo Kikuu cha Egerton.Hata hivyo, mambo hayatakuwa rahisi kwa wakili huyo kutoka Nakuru ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kisii.

Atakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Muiga Rugara, mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Jomo Kenya (JKUAT) na Katibu Mwandalizi anayeondoka Dkt Richard Bosire (UoN).Katika hali isiyotarajiwa, Bi Nyongesa amependekezwa na mwenyekiti aliyeongoza muungano huo kwa muda mrefu Bw Muga K’Olale, ambaye amekataliwa na uwakilishi wa Uasu Egerton.

  • Tags

You can share this post!

Mat Ryan hatua moja kutua Real Sociedad

Wanavyokabili janga la plastiki jiji kuu