• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 1:14 PM
Vikosi vya ujasusi, EACC kuwa macho usajili wa makurutu wa jeshi ukianza

Vikosi vya ujasusi, EACC kuwa macho usajili wa makurutu wa jeshi ukianza

Na KALUME KAZUNGU

Naibu Mkuu wa Majeshi Jonah Mwangi amezindua zoezi la kitaifa la kuajiri makurutu kujiunga na Jeshi la Kitaifa katika Makao Makuu ya Jeshi, Nairobi leo Agosti 28, 2023.

Kulingana na taarifa, kutakuwa na vituo 374 vya kupekua na kusajili makurutu kote nchini na ambavyo vitafanya zoezi hilo hadi Septemba 8.

Vikosi vya ujasusi na vile vya tume ya kupambana na ufisadi (EACC) vitakuwa katika vituo hivi kufuatilia na kunasa shughuli zozoze za kihalifu katika usajili huo.

Watu wote walio na vigezo vilivyowekwa wameshauriwa kufika kwenye vituo kujaribu bahati yao.

“Hii wala hata si kazi, huu ni wito wa kutumikia kwa kujitolea. Fika tu iwapo uko tayari kutumikia taifa lako,” akasema Naibu Mkuu wa Majeshi Jonah Mwangi.

Serikali imesema itabana idadi kamili ya watakaochukuliwa.

  • Tags

You can share this post!

Dini ya Akorino yaanza msako wa waumini wanaobugia pombe na...

Walevi, wamiliki baa Murang’a wampimia hewa Gavana...

T L