• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Wakenya kuendelea kununua unga wa mahindi kwa bei ghali

Wakenya kuendelea kununua unga wa mahindi kwa bei ghali

NA BARNABAS BII

WATEJA wataendelea kugharimika zaidi ili kununua unga kutokana na uhaba wa mahindi katika masoko ya humu nchini na ya kimaeneo licha ya serikali kuondoa ada na ushuru wa nafaka inayoagizwa kutoka nje ya nchi.

Wamiliki wa viwanda vya kusaga unga na wateja jana walisema kuondolewa kwa ushuru na ada zinazotozwa mahindi yanayoagizwa kutoka nje, kutapunguza bei ya mazao hayo kwa kiasi ‘kidogo mno.’

Hii ni kutokana na changamoto za kusaka nafaka ya kutosha kustawisha shughuli kwa miezi mitatu ijayo kabla ya mazao mengine kuwa tayari.

“Japo tunafurahia kuondolewa kwa ada zinazotozwa mahindi yanayoletwa nchini, ni mapema mno kukadiria ni kwa kiasi gani bei ya unga itapungua tukizingatia uhaba wa mahindi katika masoko ya humu nchini na ya kimaeneo,” alisema Mwenyekiti wa Muungano wa Viwanda vya Unga (GBMA), Bw Kipngetich Mutai.

Bei ya mahindi imeongezeka pakubwa huku gunia la kilo 90 likiuzwa Sh6,200 kutoka Sh5,400 wiki mbili zilizopita na kulazimu viwanda vingi kusitisha shughuli ili kuepuka gharama.

Waziri wa Kilimo, Bw Peter Munya, katika notisi iliyotolewa mnamo Julai 1, alifutilia mbali ada na ushuru unaotozwa mahindi yanayoagizwa humu nchini kwa muda wa siku 90 kuanzia Julai 1.

Hatua hiyo ililenga kuwakinga wenye viwanda na wateja kutokana na uhaba wa mahindi na kusaidia kupunguza bei ya unga.

  • Tags

You can share this post!

Mshukiwa wa wizi auawa mtaani South B polisi wakifanikiwa...

Raila akunja mkia kuhusu vyama tanzu

T L