• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 1:14 PM
Wakora wavamia akaunti za Vyombo vya Habari na kuchapisha taarifa za kupotosha

Wakora wavamia akaunti za Vyombo vya Habari na kuchapisha taarifa za kupotosha

Na SAMMY WAWERU

WAHUNI wamevamia akaunti za vyombo vya habari, na kuchapisha habari za kupotosha. 

Katika visa vya hivi punde, Gazeti la Daily Nation linalomilikiwa na Shirika la Habari la Nation Media Group (NMG) akaunti ya Twitter yenye utambuzi sawa na ile halali pamoja na ya runinga ya Citizen (Royal Media Services), mashirika hayo mawili yameathirika.

Kinyume na Twitter ya Nation.Africa ya habari chipuka yenye ufuasi zaidi ya milioni 1.7, akaunti bandia imechapisha taarifa ya runinga ya Citizen kufunga Twitter yake kwa muda hadi pale suala la akaunti zingine feki za shirika hilo litatuliwa.

Nayo akaunti bandia ya Citizen TV, imepakia habari ya Rais William Ruto, inayodai ametoa amri kukamatwa kwa waliosusia kulipa mkopo wa Mpango wa Fedha za Hastla na Ufadhili wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu.

Chapisho la ukurasa bandia wa runinga ya Citizen, limeandamanishwa na picha ya Dkt Ruto akikagua gwaride la heshima la wanajeshi (KDF).

Twitter ya Citizen TV ina zaidi ya ufuasi milioni 5.2.

Mashirika hayo mawili ya habari, yametoa taarifa kwa umma yakiitaka kupuuzilia mbali akaunti hizo.

Wahuni wadukuzi wa mitandao ya kijamii, wamekuwa wakiandama vyombo vya habari kwa kufungua kurasa feki (Twitter na Facebook) na kueneza habari potovu.

 

 

 

 

  • Tags

You can share this post!

Wanabodaboda: Hatutashiriki maandamano ya Azimio

Vincent Kompany na Mauricio Pochettino miongoni mwa...

T L