• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Wakulima wasambaziwa mbegu za alizeti kusaidia kupunguza bei ya mafuta ya kupikia

Wakulima wasambaziwa mbegu za alizeti kusaidia kupunguza bei ya mafuta ya kupikia

EVANS JAOLA na LABAAN SHABAAN

SERIKALI imezindua mpango wa kitaifa wa kuvumisha kilimo cha alizeti (Sunflower) katika mikakati ya kuinua uzalishaji wa mafuta ya kupikia.

Program hii inalenga kuganga bei ya juu ya mafuta ya kupikia inayoshuhudiwa nchini.

Jumanne, Oktoba 17, 2023, Mamlaka ya Chakula na Kilimo (AFA) ilitoa tani 70, 000 za mbegu ili kukuza kilimo cha alizeti.

Mbegu hizo za thamani ya Sh 987 milioni zitatolewa kwa wakulima wa kaunti 24 bila malipo.

Miongoni mwa kaunti zitakazofaidika ni Trans Nzoia, Bungoma na Uasin Gishu.

Kwa mujibu wa Katibu wa Wizara ya Kilimo Dkt Paul Rono, kwa sasa Kenya inazalisha mafuta ya kupikia tani 80, 000 kwa mwaka.

Dkt Rono, aliyezindua mpango huu katika kiwanda cha mbegu ya alizeti  mjini Kitale, alieleza nchi huagiza mafuta ya kupikia tani 900,000 kwa Sh117 bilioni kila mwaka.

Kiwango hiki ni cha chini kwa sababu kilimo cha alizeti kimedidimia.

“Usambazaji wa mbegu za alizeti bila malipo kwa wakulima kote nchini ni mwanzo wa kampeni kabambe ya kuimarisha uzalishaji na kudhibiti uagizaji kutoka nje,” Dkt Rono alisema.

“Kenya ina mashamba ya kutosha ya kuzalisha malighafi ya kutengeneza mafuta ya kupikia na malisho ya mifugo ili kupunguza gharama ya kuyanunua kutoka nchi za nje,” aliongeza.

AFA na magatuzi yatashirikiana kusambaza mbegu hizi yakishikana mkono na Kampuni ya Mbegu ya Kenya (KSC).

Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya alisema kaunti yake inalenga kutumia shamba ekari 20 000 katika kilimo hiki huku ekari 425 zikiwa zinatumiwa sasa.

“Baada ya kuvuna mahindi, pandeni alizeti kabla ya msimu ujao wa upanzi na hii itasaidia kuimarisha rutuba ya udongo na mapato,” Bw Natembeya aliambia wakulima.

  • Tags

You can share this post!

Ruweida Obo apendekeza maafisa wa KDF waruhusiwe kuabiri...

Mwanamume aliniomba penzi, kabla sijamjibu asharukia na...

T L