• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
Wanafunzi Thika wanufaika na basari za Sh10 milioni

Wanafunzi Thika wanufaika na basari za Sh10 milioni

NA LAWRENCE ONGARO

WANAFUNZI wapatao 2,000 kutoka eneo la Thika Mashariki mnamo Jumatatu walinufaika na basari za Sh10 milioni kutoka kwenye mfuko wa fedha za ustawi wa maeneo za NG-CDF.

Mbunge wa Thika Bi Alice Ng’ang’a, alielezea furaha yake akisema wanafunzi watanufaika pakubwa.

Kulingana na jinsi ilivyopangwa, wanafunzi walio vyuoni wanapata kiwango cha Sh8,000.

Wanafunzi walio katika shule za mabweni wataridhika na Sh6,000, huku walio katika shule ya kutwa wakinufaika na Sh4,000.

Lakini wanafunzi walio na changamoto wakiwemo wanaoishi na ulemavu walipokea Sh10,000.

Kwa sababu mara nyingi fedha hizo haziwezi zikatosheleza mahitaji yote ya karo, aliahidi kuzungumza na serikali kuu ili kuona ya kwamba muhula ujao mambo yanabadilika kwa kuongeza fedha zaidi.

“Ninajaribu kadiri ya uwezo wangu kuona ya kwamba kila mwanafunzi anapokea kiwango kifaacho ili kigharimie karo bila matatizo,” alifafanua mbunge huyo.

Alisema hivi karibuni watapokea kipande cha ardhi cha ekari 100 ambacho kilitolewa na kampuni ya Delmonte.

“Iwapo tutapata kipande hicho cha ardhi, tutafanya juhudi kuona ya kwamba kunajengwa taasisi kwenye ardhi hiyo ili wanafunzi wapate kujifunza kozi za kiufundi. Tunataka wanafunzi watakaohitimu vizuri watafutiwe kazi ya kuwakimu ili wajiendeleze kimaisha,” alisema mbunge huyo.

  • Tags

You can share this post!

Kocha Beldine Odemba kuongoza Rising Starlets kwenye...

Waendeshaji wa baiskeli walilia Mama wa Taifa wakimtaka...

T L