• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Kocha Beldine Odemba kuongoza Rising Starlets kwenye mashindano ya CECAFA

Kocha Beldine Odemba kuongoza Rising Starlets kwenye mashindano ya CECAFA

NA TOTO AREGE

KOCHA wa timu ya taifa ya Kenya ya wanawake ya Rising Starlets ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 Beldine Odemba, ataongoza timu hiyo katika mashindano ya Baraza la Mashirikisho ya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambayo yanatarajiwa kung’oa nanga kuanzia Juni 24, 2023 jijini Nairobi.

Haya yanajiri baada ya Odemba kuongoza majaribio ya kitaifa ya mchujo jijini Nairobi, katika Shule ya Wasichana ya Butere (kanda ya Magharibi), katika uwanja wa michezo wa Jomo Kenyatta (maeneo ya Nyanza) na katika uwanja wa Shanzu TTC (Pwani) mapema Mei 2023.

Majaribio hayo yalilenga kuchagua wachezaji watakaoiwakilisha nchi katika michuano hiyo.

Mshambulizi wa timu ya Ulinzi Starlets inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL) Fasila Adhiambo na Ivy Chepkirui wa Zetech Sparks ndio wachezaji wenye uzoefu zaidi ambao wamejumuishwa kwenye kikosi hicho.

Kiungo wa kati wa Soccer Assassins FC (Divisheni ya Kwanza) Rebecca Kwoba pia ni sehemu ya kikosi cha wachezaji hao 44.

Kipa Patience Kasichana na mshambulizi Shihafu Askonita kutoka Shule ya Mseto ya Dagoretti kutoka jijini Nairobi waliitwa kwa mara ya kwanza.

Askonita alikuwa sehemu ya timu ya soka ya Dagoretti iliyowakilisha Kenya katika Michezo ya Afrika Mashariki ya Shule za upili nchini Tanzania mwaka 2022.

Wachezaji hao wanatarajiwa kuingia kambini Alhamisi, Juni 8, 2023.

Makipa

Christine Omolo, Scoria Awuor, Terry Okova, Velma Auma, Shihafu Askonotia.

Mabeki

Robai Nelma, Vidah Okeyo, Judith Okumu, Dorcas Glenda, Beryl Achieng, Sharlot Atieno Obondi, Philomena Syombua, Claire Meris, Junedezina Awino, Lorine Ilavunga, Sharon Omwangale na Ruth Akinyi.

Viungo

Rebecca Kwoba, Jane Hato, Lorna Faith, Sheila Awuor Ouma, Eunice Atieno Odemba, Ephy Atieno Onyango, Susan Akoth, Jerrine Adhiambo, Jane Njeri, Velma Kaveza, Sheila Kaare Wanjiru, Conny Anyego, Sheila, Erika Njeri na Rebecca Odato.

Washambulizi

Mollviine Achieng Owour, Elizabeth Mideva, Fasila Adhiambo, Immanuela Nafula, Valerie L Nekesa, Ivy Chepkirui, Winnie Wangeci, Margaret Njeri, Patience Kasichana, Inna Akinyi, Margaret Aluoch Onyango na Edna Wanda.

  • Tags

You can share this post!

Dawa ya dawa za kulevya ni mbwa wa kunusa – Kamishna

Wanafunzi Thika wanufaika na basari za Sh10 milioni

T L