• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 3:16 PM
‘Wanajeshi 11 walioangamia kwenye ajali ya helikopta walikuwa wamejitolea kikamilifu’

‘Wanajeshi 11 walioangamia kwenye ajali ya helikopta walikuwa wamejitolea kikamilifu’

Na MARY WAMBUI

WANAJESHI 11 walioangamia katika ajali ya helikopta walipokuwa wakifanya mazoezi ya kijeshi walitajwa kama mashujaa kwa huduma yao kwa taifa katika Operesheni Linda Nchi, nchini Somalia.

Katika kisa cha kuhuzunisha, mashujaa hao walinusurika vita vikali dhidi ya wanamgambo wa al-Shabaab na kuangamia nyumbani walipokuwa wakifanya mazoezi ya kijeshi.

Maisha ya wanajeshi hao waliokuwa wametuzwa kwa medali za Operesheni Linda Nchi na za kikatiba, yalikatizwa ghafla mnamo Juni 24, 2021 helikopta waliyokuwa wakitumia aina Mi171E, ilipoanguka katika eneo la Ol Tepesi, Kaunti ya Kajiado, saa tatu asubuhi.

Mashujaa hao tisa ni Joshua Obare Odera (Warrant Officer 2), Tarcisio Wandera Namboka (Warrant Officer 2), Sajini Mkuu Noah Wanyonyi Munialo, Bob Kipkemoi Aruasa na Anthony Simon Kamuti.

Sajini Steve Ombuka Angwenyi, Stephen Omarian Omale, Corporal Boniface Ogati Mocheche na Superintendent Thomas Shekeine, watakumbukwa kwa mchango waliotoa katika Oparesheni Linda Nchi iliyokuwa ya kwanza kabisa ya wanajeshi wa Kenya Somalia 2011.

You can share this post!

Mpango wa Willian kujiunga na Inter Miami watibuka baada ya...

Nusu ya Wakenya hawajui chochote kuhusu BBI – Ripoti